Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Yatangaza Sehemu Mpya Kwaajili ya Magroup

Sasa utaweza kusoma meseji zote ulizotajwa ndani ya Group
WhatsApp Yatangaza Sehemu Mpya Kwaajili ya Magroup WhatsApp Yatangaza Sehemu Mpya Kwaajili ya Magroup

Hivi karibuni Facebook ilipata pengo baada ya mgunduzi wa WhatsApp na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa WhatsApp Jan Koum kutangaza kuachana na kampuni hiyo, ni wiki chache zimepita na sasa Facebook imesha mpata mkurugenzi mtendaji mwingine kwaajili ya kuiongoza WhatsApp. Mkurugenzi huyo aitwaye Chris Daniels anatokea Internet.org sehemu nyingine inayo milikiwa na kampuni ya Facebook.

Sasa baada ya mkurugenzi huyo kuanza kuiongoza WhatsApp, Hivi leo WhatsApp kupitia blog yake imetangaza ujio wa sehemu mpya kwaajili ya magroup. Sehemu hizo mpya zitawawezesha watumiaji wa WhatsApp kutumia sehemu ya magroup kwa namna ya kipekee na kwa urahisi zaidi.

Advertisement

Maboresho hayo ni pamoja na Group DescriptionAdmin controlsGroup catch up, pamoja na Participant search. Tukianza na Group Description, hii ni njia mpya ambayo utaweza kuweka maelezo ya Group ikiwa pamoja na sheria za group au maelezo yoyote ya muhimu kuhusu group ambayo ungependa washiriki waweze kuona kabla na baada ya kujiunga na Group. Kutumia sehemu hiyo, ingia kwenye Group husika, bofya juu kwenye jina la group, kisha chini ya jina la group bofya Add group description.

Kwa upande wa Admin controls, hii ni sehemu mpya inayo patikana kwa ma-admin au wasimamizi wa magroup ambapo sasa ma-admin wataweza kuchagua ni nani ataweza kubadilisha, picha ya group, maelezo ya group (group description) pamoja na jina la group. Awali mtu yoyote alikuwa na uwezo wa kubadilisha vitu hivyo bila hata yeye kuwa admin. Kupata sehemu hiyo ingia kwenye group husika kisha bofya juu kwenye Jina la group, kisha shuka chini kidogo utaona Group Settings, kisha bofya Edit group info, kisha badilisha kutoka All participants kwenda Only admins bofya ok.

Kwa upande wa sehemu ya mpya ya Group catch up, hii ni sehemu mpya itakayo kuwezesha kupata ujumbe au meseji zote ulizotumiwa kwenye group kwa kutajwa au kuwa mention kwa kutumia mfumo ule wa kuandika jina la mtu kwa kuanza na alama @. Sasa sehemu mpya itakuwepo kwenye group ambayo itapatikana chini upande wa kulia ambayo ndio itakuwa ikionyesha jumbe zote ulizotumiwa kwa kutajwa kwa kutumia mfumo ule wa kuanza na alama @.

Sehemu nyingine ni Participant search, hii ni sehemu mpya kwaajili ya magroup ambapo utaweza kutafuta jina la mtumiaji au watumiaji kwa urahisi zaidi. Sehemu hii inapatikana kwa kuingia kwenye group husika kisha bofya jina la group kwa juu, Kisha shuka mpaka chini kidogo angalia upande wa kulia utaona sehemu mpya yenye alama ya kutafuta bofya hapo kisha utaweza kutafuta jina la mshriki yoyote ndani ya group. Awali ilikuwa ni lazima kupitia jina la washiriki mmoja mmoja ili kupata jina la mtu unaye mtafuta kwenye group.

Mbali na sehemu hizo, sasa sehemu ile ya ma-admin kuweza kuwavua uwezo wa kuwa admin, ma-admin wenzao sasa inapatikana ndani ya programu hiyo ya WhatsApp. Ma-admin wataweza kumvua mtu yoyote uadmin kwa kubofya huku unashikilia jina la admin mwenzako kisha bofya Dismiss as admin na admin huyo atakuwa mtumiaji wa kawaida na sio tena admin.

Vilevile WhatsApp imetangaza kuwa imeleta maboresho ya ulinzi kwenye magroup ambapo sasa ukitolewa kwenye group au ukiondoka kwenye group fulani hutoweza kujiunga tena na group hilo baadae. Sehemu hizi zote tayari zimesha anza kupatikana kwenye programu za WhatsApp za iOS na Android, unaweza kujaribu sasa sehemu hizi. Kama bado ujaona sehemu hizo hakikisha una pakua toleo jipya la WhatsApp kupitia masoko husika ya App Store pamoja na Play Store.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use