Mkutano wa Facebook F8, ni mkutano ambao unafanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1 ya mwezi May hadi tarehe 2 ya mwezi huo huo, hapo ndipo wabunifu wote wa programu mbalimbali ujumuika pamoja na kujua ni nini kitakucho badilika kwenye programu zote zinazomilikiwa na Facebook yaani WhatsApp, Facebook pamoja na Instagram.
Mbali na wabunifu kujua nini kitakacho badilika kupitia mkutano huo, Facebook pia hutumia nafasi hiyo kutangaza mabadiliko mapya yanayo tegemewa kuja kwenye programu zake hizo. Mwaka huu Facebook imetangaza mambo mengi sana kwenye programu zake za Facebook, WhatsApp pamoja na Instagram, lakini kwa kuanza Hapa tutaenda kuangalia sehemu mpya ya kufauta mpenzi ndani ya mtandao wa Facebook.
Sasa hapo jana kupitia mkutano huo wa F8 (2018), Mark Zuckerberg alitangaza ujio wa sehemu maalum ambayo itakuwezesha kutafuta mpenzi au mchumba. Kupitia sehemu hiyo utaweza kutengeneza ukurasa maalum ambao utakuwa ni maalum tu kwaajili ya kutafuta mpenzi na kizuri ni kwamba, ukurasa huo utakuwa unajitenga kabisa na ukurasa wako wa kawaida wa Facebook.
Ili kujiunga na huduma hiyo, watumiaji wanatakiwa kubofya sehemu maalum ya moyo iliyoko juu upande wa kulia, kisha utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa maalum unao-itwa ‘dating home’, ukurasa huu hautakuwa unaonekana kwa marafiki zako hivyo unaweza kutumia sehemu hiyo kwa siri bila marafiki zako kuweza kujua.
Baada ya kuingia kwenye ukurasa huo, utaweza kutengeneza profile maalum au uwanja maalum kwaajili ya kutafuta mpenzi au mchumba, alafu baada ya hapo utaweza kuanza kutumia sehemu hiyo moja kwa moja.
Kwa upande wa matumizi, sehemu hiyo itajikita zaidi kwenye upande wa matamasha (Event) mbalimbali au magroup mbalimbali. Yaani unacho takiwa kufanya ni kuangalia matamasha yatakayo fanyika karibu na wewe, baada ya wewe kujisajili kwenye matamasha hiyo, utapewa uwezo wa kuangalia watu wengine walio jisajili kwenda kwenye tamasha hilo na ndani yake, utaweza kuangalia kurasa zao mbalimbali na hapo kama kuna mtu yoyote ambaye ataku-vutia basi utaweza kuanza kuchati naye moja kwa moja.
Kwa mujibu wa Facebook, sehemu hiyo ya kuchati itakuwa tofauti kabisa na sehemu ya kawaida ya kuchati kwenye mtandao wa facebook na pia itakuwa tofauti na Facebook Messenger kwa wale wanaotumia simu za mkononi. Sehemu hii inategemewa kuanza kutumika kwa majaribio miezi michache inayokuja na baadae mwaka huu itawezeshwa kwa watumiaji wote.
Mkutano wa F8 (2018) bado unaendelea kwa siku moja, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote ya muhimu yatakayo jiri kwenye mkutano huo.