Hatimaye Kampuni ya Cambridge Analytica Yatangazwa Kufungwa

Hatimaye kampuni hiyo imatengaza kufilisika kutokana na kupoteza wateja wake
cambridge-analytica cambridge-analytica

Miezi michache baada ya kuhusishwa na kashfa nzito ya uvujishaji wa data za watumiaji wa mtandao wa Facebook, hatimaye kampuni ya Cambridge Analytica imetangaza rasmi kusitisha huduma zake. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, Kampuni mama ya Uingereza inayo isimamia kampuni ya Cambridge Analytica inayojulikana kama SCL Group na yenyewe inatarajia kusitisha huduma zake ikiwa pamoja na kutangaza kufilisika.

Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa na Cambridge Analytica kwa waandishi wa habari inasema kuwa, baada ya kashfa iliyotokea baina yake na kampuni ya Facebook, karibia wateja wake wote pamoja na wasambazaji wamekuwa wakisitisha kufanya kazi na kampuni hiyo kitendo kilichofanya kampuni hiyo kufilisika na kufikia uamuzi huo mgumu wa kutangaza kufunga kampuni hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Cambridge Analytica, Alexander Nix, yeye alisha jiuzulu miezi michache liyopita baada ya kuripotiwa zaidi na wapelelezi wa siri wa habari, akijadili njia za za hatari za kusaidia kushinda kisiasa kinyume na sheria.

Advertisement

Unaweza kuangalia hapo chini video iliyo rekodiwa na waandishi hao kwa siri wakati kiongozi huyo alivyokuwa akieleza njia hizo za kushinda uchaguzi kinyume na sheria.

Kwa upande wa kampuni ya Facebook, Mara baada ya mkurugenzi wake Mark Zuckerberg kuhojiwa na Congress mwezi uliopita, sasa Facebook imejikita kuhakikisha inalinda data za watumiaji wake kwa kuleta sheria kali za utumiaji wa mtandao huo hasa kwa wabuni wa programu, ikiwa pamoja na kuleta njia mbalimbali za kiusalama ndani ya mtandao huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use