Tofauti na ilivyodhaniwa kwenye tetesi mbalimbali za ujio wa simu hii, Kampuni ya Samsung siku ya leo imezindua simu yake mpya ya Samsung Galaxy S Light Luxury, simu ambayo awali ilikuwa ikizaniwa kuja kwa jina la Galaxy S8 Lite. Simu hii mpya ya Galaxy S Light Luxury inakuja na muundo sawa na muundo wa Galaxy S8 na inakuja na kioo cha inch 5.8 chenye teknolojia ya Infinity Display kama ilivyo Galaxy S8.
Samsung Galaxy S Light Luxury inakuja na processor ya Snapdragon 660 chipset ambayo itakuwa na uwezo sawa na simu ya Galaxy S8, simu hii pia inakuja na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64, Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.
Sifa za Samsung Galaxy S Light Luxury
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.8 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, 18.5:9 ratio (~426 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260), Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 512
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa memory card hadi ya GB 400
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/1.7, 25mm, 1/3.6″, 1.22µm), autofocus.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.7, 1.12µm), phase detection autofocus pamoja na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, aptX pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Burgundy Red na Black Night.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack, Inayo uwezo wa kuzuia Maji na Vumbi.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma) na Iris scanner (Kufungua simu kwa uso).
Bei ya Samsung Galaxy S Light Luxury
Samsung Galaxy S Light Luxury inapatikana kwa nchini China pekee na simu hii inategemewa kuanza kuuzwa kwa Yuan ya China CNY 4,000 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 1,430,000. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa Tanzania kwa sababu ya kodi pamoja na kupanda kwa viwango vya kubadilisha fedha.
Unaonaje simu hii mpya ya ukilinganisha sifa za Samsung Galaxy S8 na sifa za simu hii je unaona kama sifa za simu hizi zinafanana..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.