Apps# 11 Jaribu App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Kama unatafuta App nzuri za Android Basi hapa ndio mahala sahihi.
App nzuri za Android Leo App nzuri za Android Leo

Karibu kwenye makala nyingine ya App nzuri za kujaribu kwenye simu ya Android, Kama wewe ndio mara yako ya kwanza kusoma makala hii basi ni vyema utambue kuwa kila wiki tunapata nafasi ya kukuletea App nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android. App hizi zinaweza kukusaidia kurahisisha maisha yako au matumizi ya simu yako ya Android kwa ujumla. Basi bila kupoteza muda twende tuka angalie App nzuri za wiki hii.

1. CamFind – Visual Search Engine

CamFind
Price: Free

CamFind ni App nzuri sana ya kukuwezesha kupata vitu unavyo vipenda, App hii inakusaidia pale unapoona kitu ambacho pengine unataka kujua ni shilingi ngapi au kinauzwa wapi basi unaweza kufungua App hii na kupiga picha kitu hicho kisha app hii itakuonyesha kitu hicho kinauzwa shilingi ngapi na kinauzwa wapi.

Advertisement

2. Duplicates Cleaner

Duplicates Cleaner
Price: Free

Duplicates Cleaner ni App nzuri sana ya kukusaidia kupanga simu yako vizuri, Kama kwenye simu yako kuna majina yaliyojirudia, picha, nyimbo au hata Video basi app hii itakusaidia kufuta vitu hivyo vilivyo jirudia na kuacha simu yako ikiwa na picha, majina au nyimbo za aina moja yaani ambazo hazija jirudia.

3. Khan Academy

Khan Academy
Price: Free

Khan Academy ni App nyingine nzuri sana kwa wale ambao wanapenda kujifunza mambo mapya, App hii haina matangazo na inakuruhusu kujifunza vitu kama hesabu, uchumi na mambo mengine mengi. Hivi karibuni App hii imetambuliwa na Google kama App bora kwaajili ya kujifunza.

3. Dashlane Free Password Manager

Kama wewe umekuwa unatumia password mbalimbali kwenye mitandao mbalimbali na tovuti basi app hii ni nzuiri sana kwako, App hii itakusaidia kuweza kuhifadhi password zako zote kwenye application moja, App hii itakurahisishia kutoweza kusahau password zako tena. Unaweza kutumia app hii kwenye simu pamoja na kompyuta.

4. SoloLearn: Learn to Code for Free

Solo Learn hii ni App nyingine kwaajili ya kujifunza, lakini tofauti ya App hii ni kuwa itakufundisha kuwa mtaalamu wa maswala ya programu yaani utaweza kutengeneza tovuti pamoja na programu mbalimbali ikiwa pamoja na app za Android na iOS.

5. Water Drink Reminder

Water Drink Reminder

Maji yana umuhimu sana mwilini, lakini wengi wetu tumekua tukiangalia simu zetu mara nyingi kuliko hata tunavyo kunywa maji. Sasa app ya Water Drink Reminder itakusaidia kukumbuka kunywa maji ikiwa pamoja na kiasi cha maji unachotakiwa kunywa kwa siku. App hii nzuri sana na itakusaidia kuepukana na magonjwa mbalimbali.

6. Ada – Your Health Guide

Tukiwa bado tuko kwenye upande huo huo wa Afya, Kama umekua ukijisikia vibaya mara kwa mara na hujui cha kufanya basi App ya Ada ni App nzuri sana kwako. App hii itakusaidia kuweza kujua dalili za ugonjwa mbalimbali ushauri mbalimbali wa kiafya pamoja na njia mpya ya kuweza kupata ushauri wa kidaktari bure kupitia simu yako ya mkononi.

Na hizo ndio App nilizo kuandalia kwa siku ya leo, Kama ulipitwa na App nzuri za wiki iliyopita unaweza kusoma hapa. Kama una maoni ushauri au unajua App yoyote nzuri unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

2 comments
  1. Nimekua nikifungua maelekezo mfano Apps za kujalibu kwenye simu
    nikifungua maelezo tu ndio nayakuta picha hazifunguki zinakuwa error.
    labda hii inatokana na nini

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use