Ni kweli kuwa wengi wetu tunazo simu za mkononi, lakini kila mtu anajua jinsi anavyo itumia simu yake kwa namna yake ya kipekee. Sasa wiki iliyopita msanii wa muziki John Legend yeye ametuonyesha matumizi simu ya mkononi ambayo matumizi hayo ndio yamepelekea mimi kuandika makala hii.
Msanii huyo ambaye anajulikana kwa Nyimbo kali kama, All of Me ya mwaka 2013 au Love me Now ya mwaka 2016 ametumia simu ya mkononi aina ya Google Pixel 2 kutengeneza video nzima ya muziki ya kichupa chake kipya cha A Good Night ambacho ameshirikiana na msanii, muandishi pamoja na Producer anaye julikana kwa jina la kisanii BloodPop au jina kamili Michael Tucker.
Kwa muonekano huo ni wazi kuwa walio kuwa wanatumia simu hiyo kuchukua video hii ni wataalamu sana kwani unaona jinsi video hiyo ilivyotulia. Hata hivyo simu ya Google Pixel 2 inasemekana kuwa ni moja kati ya simu zenye kamera nzuri sana ambayo inaweza kuchuna na Galaxy S9, japo mimi kwa upande wangu nakataa kuhusu hili, anyway tuache hii iwe topic ya siku nyingine.
Sasa kama umekuwa na simu yenye kamera ambayo kwa upande wako unaona ni simu yenye kamera nzuri je unaitumiaje..? Amka sasa fursa ndio hizo hata John Legend amekuonyesha kuwa, kila kitu kipo mbele yako ukichanganya na mtandao wa YouTube ambao ni bure kabisa kutumia pamoja na pia unaweza kutengeneza pesa kwa kuweka video zako ulizo zichukuwa kwa kutumia simu yako ya mkononi. Amka sasa acha kupiga Selfie na fanyia kitu cha maana kwa kutumia kamera ya simu yako.
NI SAHIHI KWAMBA UNAWEZA KUTUMIA SIMU KUTENGENEZA VIDEO LAKINI UTAFANYAJE ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YA “MB”?