Hivi karibuni tetesi zimesambaa mtandaoni kuhusu ujio wa simu mpya ya LG G7 ThinQ, Baada ya tetesi hizi kusambaa kwa muda mrefu sasa Tanzania Tech tumeona ni wakati wa kukujuza habari za tetesi hizi kwa sababu hivi leo kampuni ya LG imetangaza rasmi kuwa ni kweli itazindua simu hiyo mpya mwezi ujao wa tano tarehe 2 mwaka 2018.
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali LG G7 ThinQ itakuja na ukingo wa juu unaojulikana kama notch, ukingo ambao ulianza kuonekana rasmi mwaka jana kwenye simu mpya ya iPhone X. Tetesi hizo pia zinasema simu hiyo inakuja ikiwa na mfumo maalum wa AI au Artificial Intelligence, kama ilivyokuwa simu ya Huawei P20 na P20 Pro, ambazo nazo zilikuja na mfumo wa AI.
Hata hivyo simu hii mpya ya LG G7 ThinQ inasemekana kuja na sehemu mbayo unaweza kuficha ukingo wa juu maarufu kama notch, kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu. Kwa upande wa sifa simu hiyo inasemekana kuja ikiwa inatumia processor ya Snapdragon 845 64-bit octa-core SoC ambayo itakuwa ikisaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 4.
Simu ya LG G7 ThinQ inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au zaidi pamoja na GB 32 kwani simu hiyo inasemekana kuja zikiwa za aina mbili ambapo moja ndio itakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au zaidi na nyingine yenye ukubwa wa ndani wa GB 32.
Hata hivyo inasemekana kutakuwa na matamasha mawaili ya uzinduzi wa simu hii, tamasha la kwanza litafanyika huko nchini marekani tarehe 2 mwezi may 2018, na tamasha lingine litafanyika siku ya tarehe 3 huko Seoul, Korea kusini ambapo ndio makao makuu ya kampuni ya LG yalipo.
Vilevile simu hizi zitakuja zikiwa na rangi tano tofauti, rangi hizo ni pamoja na “Aurora Black,” “Platinum Grey,” “Moroccan Blue,” “Moroccan Blue (Matte)” pamoja na “Raspberry Rose.” kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu. Kujua zaidi kuhusu uzinduzi wa simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech.