in

Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2

Tablet hii imetengenezwa maalum kushindana na Apple iPad Pro

Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2

Kampuni ya HP hapo jana imetangaza ujio wa Tablet yake mpya ya HP Chromebook x2, Tablet hii imetengenezwa maalum kwaajili ya kuchuana na iPad Pro kwani sifa na muonekano wake zinashindana sana na zile sifa za iPad Pro.

Tablet hii ya HP Chromebook x2 inakuja na kioo cha inch 12.3 na pia inakuja na kibodi maalumu na vyote hivyo kwa bei rahisi kuliko ile ya iPad Pro, sasa kama unataka kibodi ya iPad Pro itakubidi kulipa zaidi tofauti na tablet hii mpya ya HP Chromebook x2.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tablet hii ya HP Chromebook x2 inakuja na processor za Kaby Lake chips ambazo ni Core m3 processor kutoka kampuni ya Intel’s. Kwa upande wa RAM tablet hii inakuja na RAM ya GB 4 ambayo inaweza kuongezewa hadi RAM ya GB 8, ukubwa wa ndani wa Tablet hii unakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 ambao unaweza kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 256.

Kioo cha HP Chromebook x2 kinakuja kwa Inch 12.3 chenye resolution ya 2400 x 1600 pixel, mengineyo kwenye tablet hiyo ni pamoja na kamera ya megapixel 5 kwa mbele na kamera ya megapixel 13 kwa kamera ya nyuma. Pia tablet hii inayo sehemu ya USB ambayo ni aina ya USB Type C port na vilevile inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack pamoja na battery isiyotoka yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa masaa 10.5.

Kwa upande wa mfumo HP Chromebook x2 kama lilivyo jina lake itakuja ikiwa inatumia mfumo kutoka Google unaitwa Chrome OS ambao unakuwa umefanana sana na mfumo wa Android lakini mfumo huo huwa umeboresho zaidi kwaajili ya vifaa kama hivyo (tablet na laptop).

Kwa upande wa bei HP Chromebook x2 itakuja ikiwa inauzwa kwa bei ya dollar za marekani $599 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,360,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Tablet hii itaanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi wa sita mwaka huu kupitia maduka mbalimbali ya HP ila kumbuka bei ya tablet hii hapa Tanzania inaweza kubadilika kutokana na kodi.

Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments