Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2

Tablet hii imetengenezwa maalum kushindana na Apple iPad Pro
Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2 Kampuni ya HP Yazindua Tablet Mpya ya HP Chromebook x2

Kampuni ya HP hapo jana imetangaza ujio wa Tablet yake mpya ya HP Chromebook x2, Tablet hii imetengenezwa maalum kwaajili ya kuchuana na iPad Pro kwani sifa na muonekano wake zinashindana sana na zile sifa za iPad Pro.

Tablet hii ya HP Chromebook x2 inakuja na kioo cha inch 12.3 na pia inakuja na kibodi maalumu na vyote hivyo kwa bei rahisi kuliko ile ya iPad Pro, sasa kama unataka kibodi ya iPad Pro itakubidi kulipa zaidi tofauti na tablet hii mpya ya HP Chromebook x2.

Advertisement

Tablet hii ya HP Chromebook x2 inakuja na processor za Kaby Lake chips ambazo ni Core m3 processor kutoka kampuni ya Intel’s. Kwa upande wa RAM tablet hii inakuja na RAM ya GB 4 ambayo inaweza kuongezewa hadi RAM ya GB 8, ukubwa wa ndani wa Tablet hii unakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 ambao unaweza kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 256.

Kioo cha HP Chromebook x2 kinakuja kwa Inch 12.3 chenye resolution ya 2400 x 1600 pixel, mengineyo kwenye tablet hiyo ni pamoja na kamera ya megapixel 5 kwa mbele na kamera ya megapixel 13 kwa kamera ya nyuma. Pia tablet hii inayo sehemu ya USB ambayo ni aina ya USB Type C port na vilevile inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack pamoja na battery isiyotoka yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa masaa 10.5.

Kwa upande wa mfumo HP Chromebook x2 kama lilivyo jina lake itakuja ikiwa inatumia mfumo kutoka Google unaitwa Chrome OS ambao unakuwa umefanana sana na mfumo wa Android lakini mfumo huo huwa umeboresho zaidi kwaajili ya vifaa kama hivyo (tablet na laptop).

Kwa upande wa bei HP Chromebook x2 itakuja ikiwa inauzwa kwa bei ya dollar za marekani $599 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,360,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Tablet hii itaanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi wa sita mwaka huu kupitia maduka mbalimbali ya HP ila kumbuka bei ya tablet hii hapa Tanzania inaweza kubadilika kutokana na kodi.

2 comments
  1. Itakua vizuri sana ikija na mtindo wa kujua
    majina ya watu wanao piga simu bila majina, kama ni WI ~FI basi iwe na kifaa maalumu cha utambuzi wa calling zote

  2. Naomba mnisaidie kujua jinsi mfumo wa chromebook unavyofanya kaz maana nnayo chromebook ya accer hapa na siwez kuitumia

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use