in

Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Black Shark Kwaajili ya Game

Simu hii inakuja na mfumo mpya wa kupooza simu pale inapopata joto

Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Black Shark Kwaajili ya Game

Kama wewe ni mpenzi wa kucheza Game kupitia simu, basi ni vyema ukaifahamu simu mpya kutoka Xiaomi inayoitwa Black Shark. Hii ni simu mpya kabisa kwa wapenzi wa kucheza Game kutoka kampuni ya Xiaomi ambayo ukweli imefanya mapinduzi makubwa sana ya teknolojia hasa kwa upande wa simu zenye uwezo mkubwa wa kutumika kucheza Game.

Xiaomi Black Shark inakuja na teknolojia mpya ya kupooza simu isipate joto pale unapokua unaitumia simu hii kucheza game kwa muda mrefu na vilevile kuongeza uwezo zaidi simu hii inakuja na processor mpya ya Snapdragon 845 pamoja na battery kubwa yenye uwezo wa 4,000 mAh, mbali na hayo simu hii inakuja na GPU ya Adreno 630 GPU ambayo inasaidiwa na RAM za aina mbili kati ya RAM ya GB 6 au GB 8.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama unavyo ona hapo juu, simu hii ya Xiaomi Black Shark inakuja na mfumo makini wa kupooza simu unaojulikana kama liquid cooling system ambao unaweza kupooza CPU ya simu hiyo hadi nyuzi joto za chini ya 8 ° Celsius. Simu hii haiji na sehemu ya kuweka memory Card lakini inakuja na ukuwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128.

Upande wa teknolojia ya kioo, Xiaomi Black Shark inakuja na Kioo chenye ukubwa wa inch 5.99 chenye aspect ratio ya 18:9 pamoja na teknolojia ya IPS LCD na Full HD. Mbali na hayo simu hii inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android Oreo ambao unao mfumo wa mpya wa Xiaomi wa JOY UI.

Kwa nyuma Xiaomi Black Shark inakuja na kamera mbili zenye uwezo wa Megapixel 12 MP yenye uwezo wa f/1.75 na nyingine ya Megapixel 20 yenye uwezo wa f/1.75, 6P lens, kamera zote zinasaidiwa na Flash ya dual-LED flash. Kamera ya mbele ya simu hii inakuja na uwezo wa Megapixel 20 yenye uwezo wa f/2.2.

Kukoleza mambo na kuletea urahisi wa kutumia Xiaomi Black Shark inakuja na kichezeo au Pad maalum ya kucheza game ambayo yenyewe inakuja na uwezo wa Bluetooth pamoja na battery yenye uwezo wa 340 mAh pad hiyo inauwezo wa kuunganishwa na simu hiyo kwa haraka kwa kubofya kitufe maalumu kilichopo kwenye simu hiyo. Pad hiyo itauzwa tofauti na simu lakini wateja 50,000 wa kwanza watapewa pad hiyo bure kabisa.

Kuhusu maswala ya Bei na upatikanaji, Xiaomi Black Shark itaanza kupatikana rasmi kupitia mtandaoni kwenye tovuti ya JD.com kuanzia terehe 20 mwezi huu wa nne na itapatikana kwa rangi mbili za Polar Night Black na Sky Gray. Bei ya simu hizi inatofautiana kwani Xiaomi Black Shark ya GB 128 na RAM GB 8 itauzwa kwa Yuan ya China CNY 3,499 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,300,000 na Xiaomi Black Shark ya ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 6 yenyewe itauzwa kwa Yuan ya China CNY2,999 sawa na Tsh 1,100,000. Kumbuka bei hizo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo na kumbuka bei inaweza kubadilika.

Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Black Shark Kwaajili ya Game
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments