Simu za Samsung na Bei Zake Mwaka (2018)

Kama unatafuta simu nzuri ya Samsung Soma list hii

Samsung ni moja kati ya kampuni za utengenezaji wa simu yenye simu nyingi pengine kuliko kampuni nyingine za utengenezaji wa simu hasa za Android. Kutokana na hayo nimeona kuna uhitaji wa kuja na list hii ya simu bora za Samsung ambayo itakuwezesha kujua simu bora za kununua ndani ya mwaka huu 2018. Lakini kabla ya kuanza labda niweke wazi kuwa, kuna simu nyingi sana za Samsung hivyo tumejitahidi kufanya uchunguzi wa hali ya juu na kuja na list hii lakini pia inawezekana kuna baadhi ya simu hazipo kwenye list hii hivyo unaweza kuchangia kupitia sehemu ya maoni kama utaona kuna simu imesahaulika.

Samsung Galaxy S9 na S9 Plus

Najua hapa sina haja ya kusema sana, Simu za Galaxy S9 ni Simu nzuri sana kununua kwa sasa, simu hizi zinakuja na sifa na uwezo mzuri sana hasa kwa wale watu wanao pendelea picha au kamera yenye uwezo mkubwa. Simu hizi kwa sasa zinapatikana hapa Tanzania na unaweza kuzipata kupitia maduka mbalimbali pamoja na masoko ya mtandao. Bei ya S9 ina anzia Tsh 2,300,000 hadi Tsh 2,500,000 Simu ya Galaxy S9 Plus ina anzia Tsh 3,000,000 hadi Tsh 2,800,000.

 • Dimensions: 158.1 x 73.8 x 8.5mm
 • OS: Android 8
 • Screen size: 6.2-inch
 • Resolution: 1440 x 2960
 • CPU: Octa-core (4×2.7 GHz Mongoose M3 & 4×1.8 GHz Cortex-A55)
 • RAM: 6GB
 • Storage: 64GB/128GB
 • Battery: 3,500mAh
 • Rear camera: Dual 12MP
 • Front camera: 8MP

Samsung Galaxy Note 8

Pamoja na kwamba simu hii ilikuwa na majanga kidogo, lakini hii ni moja kati ya simu ambazo ni nzuri sana na sifa zake ni kama za S9 lakini ni tofauti kidogo kwenye upande wa kamera, Simu hii inasifa nzuri sana na uwezo wa kipekee na kama ulikuwa unatafuta simu bora ya kununua mwaka huu badala ya S9 basi hii pia ni simu nzuri sana ya kuwa nayo. Simu hii unaweza kuipata kwa Tsh 2,500,000 hadi Tsh 3,000,000.

 • Dimensions: 162.5 x 74.8 x 8.6mm
 • OS: Android 8
 • Screen size: 6.3-inch
 • Resolution: 1440 x 2630
 • CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose M2 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 6GB
 • Storage: 64GB/128GB/256GB
 • Battery: 3,300mAh
 • Rear camera: Dual 12MP
 • Front camera: 8MP

Samsung Galaxy S8 na S8 Plus

Hapa pia sina haja ya kusema maneno mengi sana, wote tunaijua simu ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus. Simu hii pia ni moja kati ya simu ya Samsung ambayo ni bora sana kuwa nayo kwani simu hii ina uwezo mkubwa sana pamoja na sifa za kipekee. Unaweza kuipta Samsung Galaxy S8 kwa Tsh 2,000,000 hadi Tsh 1,800,000. Kwa upande wa Galaxy S8 Plus utaipata kwa Tsh 2,500,000 hadi Tsh 2,050,000.

 • Dimensions: 148.9 x 68.1 x 8mm
 • OS: Android 8
 • Screen size: 5.8-inch
 • Resolution: 1440 x 2960
 • CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose M2 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 4GB
 • Storage: 64GB
 • Battery: 3000mAh
 • Rear camera: 12MP
 • Front camera: 8MP

Samsung Galaxy S7 na S7 Edge

Pamoja na kwamba imepita miaka kadhaa, lakini ukweli bado simu hii iko kwenye chat sanaa. Simu hii ni moja kati ya simu nyingine ya Samsung bora sana kuwa nayo, simu hii inauwezo wa kipekee na inasemekana mwaka huu simu hii pia inategemewa kupata toleo jipya la Android Oreo 8.0. Unaweza kupata S7 kuanzia Tsh 800,000 hadi Tsh 650,000 na S7 Edge unaweza kuipata kwa Tsh 900,000 hadi Tsh 750,000.

 • Dimensions: 142.4 x 69.6 x 7.9mm
 • OS: Android 7 – Android 8
 • Screen size: 5.1-inch
 • Resolution: 1440 x 2560
 • CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose & 4×1.6 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 4GB
 • Storage: 32GB
 • Battery: 3,000mAh
 • Rear camera: 12MP
 • Front camera: 5MP

Samsung Galaxy A8 na A8 Plus (2018)

Galaxy A8 (2018) ni moja kati ya simu zenye muundo mzuri sana, mbali ya kuwa na muundo mzuri simu hii ina sifa nzuri sana na makini. Kwa wale wanaopenda simu za samsung basi ni vyema ufahamu simu hii kwani ni moja kati ya simu bora sana yaani sana. Unaweza kuipta A8 kuanzia Tsh 1,200,000 hadi Tsh 750,000 na unaweza kupata A8 Plus kwa Tsh 1,500,000 hadi Tsh 900,000.

 • Dimensions: 149.2 x 70.6 x 8.4 mm (5.87 x 2.78 x 0.33 in)
 • OS: Android 7.1.1 (Nougat)
 • Screen size: 5.6-inch
 • Resolution: 1080 x 2220 pixels
 • CPU: Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 4GB
 • Storage: 32GB/64GB
 • Battery: 3,000mAh
 • Rear camera: 16MP
 • Front camera: Dual: 16 MP

Samsung Galaxy A7 (2017)

Samsung Galaxy A7 (2017) ni simu nyingine kutoka kampuni ya Samsung, Japokuwa simu hii ni ya mwaka mmoja ulipita lakini ukweli simu hii ni nzuri sana kwa sifa pamoja na muonekano. Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung basi hakikisha simu hii inakuwa kwenye list ya simu kama unafikiria kwenda kutafuta simu nzuri ya kununua. Unaweza kuipata simu hii kuanzia Tsh 1,200,000 hadi Tsh 600,000.

 • Dimensions: 156.8 x 77.6 x 7.9 mm (6.17 x 3.06 x 0.31 in)
 • OS: Android 8.0 (Oreo)
 • Screen size: 5.7 -inch
 • Resolution: 1080 x 1920 pixels
 • CPU: Octa-core 1.9 GHz Cortex-A53
 • RAM: 3GB
 • Storage: 32GB
 • Battery: 3,600mAh
 • Rear camera: 16MP
 • Front camera: 16 MP

Samsung Galaxy A5 (2017)

Galaxy A5 2017 ni simu nyingine kwenye mfululizo wa simu za A Series, Simu hii ni nzuri sana na ukweli inauwezo mkubwa sana. Mbali na uwezo na Uzuri wa simu hii simu hii ni bora kwa wale wanapenda simu ndogo ambazo zinashikika mkononi. Unaweza kupata simu hii kwa Tsh 800,000 hadi Tsh 600,000.

 • Dimensions: 146.1 x 71.4 x 7.9 mm (5.75 x 2.81 x 0.31 in)
 • OS: Android 8.0 (Oreo)
 • Screen size: 5.2 -inch
 • Resolution: 1080 x 1920 pixels
 • CPU: Octa-core 1.9 GHz Cortex-A53
 • RAM: 3GB
 • Storage: 32GB/64GB
 • Battery: 3,000mAh
 • Rear camera: 16MP
 • Front camera: 16 MP

Samsung Galaxy C9 Pro

C9 Pro ni simu nyingine kutoka Samsung ambayo ni bora na yenye sifa nzuri yaani kuliko baadhi ya simu za Samsung za Toleo la Galaxy S. Mbali ya kuwa na sifa nzuri simu hii ni ngumu sana na kiukweli inadumu sana. Kwa mujibu wa maoni mbalimbali simu hii ni bora zaidi kuliko hata Galaxy S8. Unaweza kuipata kwa Tsh 1,300,000 hadi Tsh 800,000.

 • Dimensions: 162.9 x 80.7 x 6.9 mm (6.41 x 3.18 x 0.27 in)
 • OS: Android 7.1.1 (Nougat)
 • Screen size: 6.0 -inch
 • Resolution: 1080 x 2220 pixels
 • CPU: Octa-core (4×1.95 GHz Cortex-A72 & 4×1.4 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 6GB
 • Storage: 32GB/64GB
 • Battery: 4,000mAh
 • Rear camera: 16MP
 • Front camera: 16 MP

Samsung Galaxy C7 Pro (2017)

Kama ilivyo C9 Pro, toleo la Samsung Galaxy C7 Pro pia ni toleo bora la simu za samsung, simu hii inatamba sana kwa kuwa na ubora wa hali ya juu. Mbali na sifa zake simu hii unaweza kudumu nayo kwa muda mrefu kutokana na ugumu wake. Unaweza kuipata C7 Pro kwa Tsh 1,200,000 hadi Tsh 900,000.

 • Dimensions: 156.5 x 77.2 x 7 mm (6.16 x 3.04 x 0.28 in)
 • OS: Android 7.0 (Nougat)
 • Screen size: 5.7 -inch
 • Resolution: 1080 x 1920 pixels
 • CPU: Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53
 • RAM: 4GB
 • Storage: 64GB
 • Battery: 3,300mAh
 • Rear camera: 16 MP
 • Front camera: 16 MP

Samsung Galaxy J7 Max (2018)

Samsung Galaxy J7 Max ni simu nyingine kutoka Samsung ambayo ukweli ni simu bora sana, simu hii inauwezo mzuri sana pamoja na muonekano mzuri. Japokuwa simu hii ni ya mwaka jana lakini naweza kukwambia kuwa bado simu hii ni simu bora sana. Unaweza kuipata simu hii kwa Tsh 700,000 hadi Tsh 650,000.

 • Dimensions: 156.7 x 78.8 x 8.1 mm (6.17 x 3.10 x 0.32 in)
 • OS: Android 7.0 (Nougat)
 • Screen size: 5.7 -inch
 • Resolution: 1080 x 1920 pixels
 • CPU: Octa-core (4×2.35 GHz Cortex-A53 & 4×1.65 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 4GB
 • Storage: 32GB
 • Battery: 3,300mAh
 • Rear camera: 13 MP
 • Front camera: 13 MP

Na hizo ndio simu za Samsung ambazo ni bora na ambazo unaweza kununua kwa sasa kupitia maduka mbalimbali yanayo uza simu za Samsung hapa Tanzania na Afrika Mashariki. Kama nilivyo sema hapo awali, list hii haina simu zote za Samsung hivyo unaweza kutuambia kwenye maoni kama kuna simu tuliyo isahau na sisi tutaweza kuongeza kwenye list hii moja kwa moja.

Tanzania Tech

Follow us @ Tanzania Tech

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 11

Toa Maoni Hapa
 1. Kwa nn sim ya s9 na s8 being zao zinalingana na zko tafaut katika matumiz hebu naomba ufafanuz kidogo kuhusu ila namba 0778998120 au 0623600187

 2. Mimi naitaji simu nzuri ya Samsung nichagulieni kati ya simu hizi zifuatazo Samsung A 5 ya mwaka 2017 na Samsung A 7 ya mwaka 2018. Pia niorodheshee bei za simu nilizozitaja, Namba yangu 0738744013, 0656974269 E mail [email protected]

 3. nawapongeza sana .kutokupoteza .nembo ya SAMSUNG .kwa juu ya kioo. sio nyuma ya kioo.

  sio mpaka mtu aniulize ^*. eti simu gani.
  inatakiwa yeye ndo usikie akisema

  %+( SAMSUNG GALAXY )+%

 4. mm sinaaa maoni ila nina swali limalosemaaaa kuwa kunatofautii gan kwenye hii simu ya A7 maama bei zake kuna ya 1200000 na 600000

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.