Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sony Yazindua Simu Mpya ya Sony Xperia XZ2 Premium

Kama wewe ni mpenzi wa simu kutoka kampuni ya Sony soma hii
Sony Yazindua Simu Mpya ya Sony Xperia XZ2 Premium Sony Yazindua Simu Mpya ya Sony Xperia XZ2 Premium

Baada ya Sony kuzindua simu yake mpya ya Sony Xperia XZ2 mapema mwaka huu kwenye mkutano wa MWC 2018, hivi leo kampuni hiyo imerudi tena ikiwa na Simu mpya ya Sony Xperia XZ2 Premium. Simu hii inakuja kama maboresho mapya ikiwa na kioo chenye teknolojia ya 4K pamoja na kamera yenye uwezo mzuri sana wa kupiga picha kwenye mwanga mdogo.

Advertisement

Kwenye maboresho ya simu hii kitu kilicho zingatiwa sana ni kamera, Simu hii ya Sony Xperia XZ2 Premium inakuja na kamera mbili kwa nyuma ambazo zinakuja na mfumo wa lensi maalum za telephoto pamoja na zoom lensi ambazo pia zinapatikana kwenye simu za Apple iPhone, Samsung, pamoja na simu za OnePlus.

Simu hii inakuja na kamera mbili zenye lensi hizo ambazo kamera moja inayo megapixel 19 ambayo hii inachukua picha zenye rangi na kuziboresha zaidi na nyingine inayo Megapixel 12 ambayo hii inachukua picha za monochrome au picha zinazo boreshwa vizuri kwenye rangi nyeusi na nyeupe.

Mbali na hayo simu hiyo ya Sony Xperia XZ2 Premium inakuja na kioo cha inch 5.8 ambacho chenyewe kinakuja na teknolojia ya 4K hii ikiwa na maana una uwezo wa kuangalia Video za HDR video kwenye simu hii, Sifa nyingine za Sony Xperia XZ2 Premium ni kama zifuatazo.

Sifa za Sony Xperia XZ2 Premium

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya IPS LC, HDR10 compliant, Triluminos display, X-Reality Engine, capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 3840 x 2160 pixels, 16:9 ratio (~760 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 kwa simu ya rangi ya Gold na  Octa-core 4×1.7 GHz Kryo 385 kwa simu ya rangi ya Silver) Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset kwa simu zote mbili.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye (f/2.0, 22mm, 1/3″, 1.12 µm), 5-axis giro EIS, pamoja na uwezo wa 1080p
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 19  yenye (f/1.8, 25mm, 1/2.3″, 1.22μm) na nyingine yenye Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.6, 1/2.3″, 1.55μm) kamera zote mbili zina teknolojia ya 5-axis gyro EIS, predictive phase detection na laser autofocus, ikiwa pamoja na Flash ya LED flash
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3540 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, Wi-Fi Direct, DLNA, hotspot aina ya USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Chrome Black na Chrome Silver
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM Haina Radio.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Bei ya simu hii ya Sony Xperia XZ2 Premium bei yake bado haija tangazwa lakini kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya Teknolojia simu hii inakadiriwa kuja ikiwa na bei ya dollar za marekani $900 au $1,000 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 2,040,000 au Tsh 2,265,000. Kumbuka bei hiyo inaweza kubadilika pale bei halisi ya simu hii itakapo tangazwa rasmi na pia bei hizo hapo juu ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Kwa habari zaidi za simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use