Mtoto wa Miaka 12 Anaeweza Kudukua Password Yoyote

Mbali na kuwa na uwezo huo, pia ni mtaalamu wa maswala ya Kung Fu
reuben Paul Cyber Ninja reuben Paul Cyber Ninja

Unaweza kudhani uko salama kutokana na kuwa na nywila au password ndefu au yenye alama na herufi zisizo eleweka, Well…. fikiria tena kwani hiyo password unayodhani ni ngumu sana mtu kuifahamu inaweza kupatikana au kudukuliwa kirahisi sana hata na mtoto wa miaka 12.

Reuben Paul ni mtoto wa darasa la sita au kwa wenzetu sixth grader, ambaye anatokea huko Austin, Texas nchini marekani. Mtoto huyu wa miaka 12 anapendelea sana akiitwa jina la “Cyber Ninja” kwani mbali na kuwa na kipaji cha kudukuwa nywila au password yoyote, pia analo taji la shahada ya pili ya mkanda mweusi kwenye maswala ya martial art au Kung Fu.

Mtoto huyo kwa sasa yupo kwenye hatua ya kutangaza kwa dunia kuhusu usalama wa mtandoni na jinsi ya kujilinda na mashambulizi ya mtandaoni. Reuban ameshawahi kusimama kwenye matamasha makubwa huko Texas nchini marekani pamoja na uholanzi akielezea jinsi ya kujilinda  kikamilifu na uhalifu wa mtandaoni. Hata hivyo kuonyesha ujuzi wake Reuban alishawahi kudukua mdoli wenye kamera na kugeuza kuwa chombo cha kurekodi sauti na video.

Advertisement

Kutokana na uwezo wake huo, tayari nchi mbalimbali kama uholanzi na wizara ya ulinzi ya marekani imeshamfuata kwa lengo la kumpa kazi mtoto huyo, lakini Reuban mwenyewe amesema anataka kumaliza shule kwanza ndipo afikirie kuhusu maswala ya kazi.

Kwa sasa Reuban au “Cyber Ninja” bado anaendelea na shule huku ndoto zake kubwa zikiwa ni kufanya kazi kwenye shirika la upelelezi la marekani (Federal Bureau of Investigation) FBI au usalama wa Taifa wa marekani (National Security Agency) NSA.

3 comments
    1. ni balaaaa. kweli app hii ni nzuri sana, naomba mnijuze nataka kununua laptop kwa ajili ya Shule chuo kikuu hasa maswala.ya statistics na finance je laptop gani nzuri zaidi kati ya dell xp 13 au macbook air 13

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use