Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae Kununua Laptop Mpya Yenye Processor ya Core i9

Processor hii mpya inayo speed mara 41 zaidi ya processor ya core i8
Processor mpya za Intel Core i9 Processor mpya za Intel Core i9

Kampuni ya Intel ambayo ni maarufu kwa utengenezaji wa Processor hivi leo imetangaza kuwa sasa imeanza kutengeneza processor za Core i9 kwaajili ya Laptop. Hapo awali kampuni hiyo ilikuwa imetengeneza processor hizo kwaajili ya kompyuta za mezani (desktop) pakee.

Hata hivyo processor hizo mpya ambazo zinasemekana kuja zikiwa na nguvu zaidi, zinategemewa kutumika zaidi kwenye kompyuta maalumu za kucheza game kutokana na uwezo wake mkubwa. Processor hizo ambazo zimepewa jina la Intel Core i9-8950HK zinakuja na speed ya hadi 4.8 GHz pamoja na teknolojia ya turbo boost, huku zaikiwa za kwanza duniani zenye uwezo wa six cores pamoja na 12 threads yaani maana yake ni kwamba processor hizi zitakuwa na speed asilimia 29 zaidi ya processor za Core i8.

Advertisement

Hata hivyo intel imeongeza kuwa processor hizo zitakuwa na uwezo wa asilimia 41 zaidi kwenye upande wa game na asilimia 59 zaidi kwenye uwezo wa ku-edit video zenye teknolojia ya 4K. Mbali na hayo kampuni ya intel pia imezindua matoleo mapya ya processor za Core i5+ na Core i7+ ambazo nazo pia zitakuja na maboresho mapya pamoja na speed zaidi.

Kwa sasa bado hakuna laptop yoyote yenye processor ya Core i9 hivyo bado tunasubiri kujua ni laptop gani itakayokuja na processor hii mpya kutoka kampuni ya Intel. Endelea kutembelea Tanzania tech tutakujuza yote pindi tu yatakapo tufikia.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use