Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Muonekano wa Simu Mpya ya Samsung Galaxy A6 (2018)

Huu ndio muonekano rasmi wa Samsung Galaxy A6 (2018)
Muonekano wa Galaxy A6 (2018) Muonekano wa Galaxy A6 (2018)

Ni siku chache zimeisha toka tukwambie kuhusu ujio wa Samsung Galaxy A6 (2018) pamoja na A6+ (2018), lakini wakati tukiwa bado tunasubiri kuzinduliwa rasmi kwa simu hii Tayari tumefanikiwa kupata muonekano wa simu hiyo mpya. Muonekano huu ndio muonekano halisi wa simu hiyo inayo tarajiwa kuzinduliwa siku za karibuni.

Kama unavyoona kwenye picha hapo juu, simu hizi zinakuja zikiwa zimetengenezwa kwa kava la chuma huku kioo chake kikiwa ni Full Display kama ilivyo simu ya Galaxy S8. Ukiangalia picha hizo kwa umakini utaona pia spika ya simu hii inatarajiwa kuwa sehemu tofauti sana na tulipo zoea kwani kama unavyo weza kuona hapo juu spika ya simu hiyo itakuwa kwa pembeni na sio juu au chini kama ilivyo zoeleka.

Advertisement

Kitu kingine ambacho kinaonekana kwenye picha hizo ni kuwa, Galaxy A6 na A6+ zitakuja na sehemu tofauti za line pamoja na Memory Card, tofauti na simu nyingi za sasa ambapo laini za simu na memory card zinakaa pamoja kwenye tray moja huku ukipewa chaguo la kutumia line ya pili au kutumia memory card.

Kwa upande wa sifa kama nilivyo kueleza awali, Simu ya Galaxy A6 (2018) inatarajiwa kuja na kioo cha inch 5.6 chenye teknolojia ya Infinity Display pamoja na resolution ya 2220 x 1080. Kwa upande wa ukubwa wa ndani A6 inategemewa kuja na GB 32 ambayo itakuwa ikisaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na Processor ya Exynos 7870 Octa chipset. Galaxy A6+ (2018) yenyewe inategemewa kuja na kioo chenye ukubwa huo huo, lakini ukubwa wa ndani utakuwa GB 64 pamoja na RAM ya GB 4 pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 625.

Tuambie unaonaje muonekano wa Samsung Galaxy A6 (2018).? je ni simu ambayo ungependelea kuwa nayo..? Tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use