in

WhatsApp Kuwezesha Kurudisha Picha na Video Zilizofutika

Utaweza kurudisha picha zilizofutika ndani ya mwezi mmoja au siku 30

WhatsApp Kuwezesha Kurudisha Picha na Video Zilizofutika

WhatsApp imekuwa ikifanya maboresho mengi sana, moja ya maboresho ya siku za karibuni ni pamoja na sehemu ya (Delete For Everyone), kama wengi wenu mnavyojua sehemu hii inakuwezesha kufuta meseji uliyo ikosea na pale unapofuta meseji hiyo, itafutika hata kwa mtu au watu uliyo watumia meseji hiyo. Sasa mbali na sehemu hiyo, kwa sasa WhatsApp inafanya majaribio ya sehemu mpya kabisa ambayo itakuwezesha kupakua kwa mara nyingine picha au video ambazo zimefutika au ulizozifuta.

Kwa mujibu wa mtandao wa WABetainfo, sehemu hiyo kwa sasa inapatikana kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta ambapo itawezesha watumiaji kupakua tena video, picha pamoja na File za aina nyingine zilizofutika ndani ya mwezi mmoja tu, hivyo kama file hizo zimefutwa zaidi ya siku 30 zilizopita hutoweza kuzipakua tena mpaka pale utakapo tumiwa tena.

Lakini pia mtandao huo umeandika kuwa files hizo, video na picha zitakazo weza kurudishwa na kupakuliwa tena ni zile ambazo zitakuwa zimefutika kwenye Gallery au File Manager ya simu yako na sio zile zilizo futwa kwenye chat zako ndani ya programu ya WhatsApp. Yaani hapa kwa kifupi ni kuwa, kama ukifuta picha wakati unachat ndani ya programu ya WhatsApp hutoweza kuzipata tena kwa kutumia sehemu hiyo, Bali kama umefuta picha hizo kwenye Gallery au File Manager basi utaweza kutumia sehemu hiyo kurudisha picha, video au file zingine.

Apps Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu Yako Mwezi #January

Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa Programu ya majaribio ya WhatsApp Beta kwa mfumo wa Android lakini inasemekana sehemu hii inaweza kuja kwa watumiaji wote siku za karibuni. Kwa habari zaidi kuhusu sehemu hii na siku itakayo kufikia kwenye programu yako ya WhatsApp endelea kutembelea Tanzania Tech.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.