Kampuni ya Samsung inajiandaa kurudi sokoni hivi karibun na simu mpya za Samsung Galaxy A6 pamoja na Galaxy A6 Plus, simu hizi zinategemewa kuja zikiwa kama toleo jipya la Simu za Samsung Galaxy A8 simu ambazo zilizinduliwa hapo mwishoni mwa mwaka jana 2017.
Ripoti kutoka kwenye tovuti ya GSM Arena zinasema kuwa, Simu hizi mpya za Samsung Galaxy A6 zinatarajiwa kuja na kioo cha inch 5.6 chenye teknolojia ya Infinity Display pamoja na resolution ya 2220 x 1080. Kwa upande wa ukubwa wa ndani A6 inategemewa kuja na GB 32 ambayo itakuwa ikisaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na Processor ya Exynos 7870 Octa chipset.
Kwa upande wa Galaxy A6 Plus yenye inategemewa kuwa na kioo chenye resolution sawa na A6 lakini yenyewe itakuwa tofauti kidogo kwenye ukubwa wa kioo kwani itakuwa na kioo cha Inch 6 ambacho kitakuwa na teknolojia ya Infinity Display. Simu hii pia inatarajiwa kutofautiana na A6 ya kawaida kwenye upande wa RAM ambapo itakuwa na RAM ya GB 4.
Galaxy A6 Plus pia itakuja na processor ya tofauti ambayo yenyewe itakuwa ni processor ya Qualcomm Snapdragon 625 au Snapdragon 450. Kwa sasa bado hakuna uhakika sana wa sifa hizi tunatumaini Samsung itazindua simu hizi siku za usoni na tutaenda kuzifahamu sifa za simu hizo kwa undani zaidi hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech.