Kampuni ya Huawei hivi leo imetangaza ujio wa soko lake jipya la App Gallery, Kampuni hiyo imetangaza kuwa sasa watumiaji wa simu za Huawei wataanza kufurahia programu za Android kupitia soko lake jipya ambalo litakua na programu mbalimbali za Android pamoja na programu maalum kwa watumiaji wa simu za Huawei.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya GSM Arena, Huawei wamenza kuweka soko hilo ndani ya simu za Huawei kuanzia simu mpya za Huawei P20 pamoja na Huawei P20 Pro, na kuanzia hapo simu zote zitakazo kuwa zinakuja sokoni zitakuwa na soko hilo ndani yake.
Huawei ni kampuni ya tatu kwa ukubwa baada ya kampuni za Apple na Samsung, lakini kampuni ya Huawei ilikuwa bado haina soko lake la programu ukilinganisha na kampuni ya Samsung ambayo ilianza kuwa na soko lake la Galaxy Apps ambalo mpaka sasa linakuja ndani ya simu zote za Samsung.
Kwa muda huu watumiaji wa simu za Huawei wataweza kupakua soko hilo la App Gallery Moja kwa moja kwenye simu zao kupitia link maalum hapo chini inayotoka kwenye ukurasa wa Soko hilo kupitia tovuti ya kampuni ya Huawei.
Kwa watumiaji wa simu nyingine ambazo zio za Huawei wanaweza kupakua programu hiyo lakini utaitajika kupakua na kuinstall programu nyingine inayoitwa Huawei Mobile Services, programu hiyo inapatikana Play Store hivyo kama unataka kujaribu soko hili jipya la App Gallery basi ni vyema kupakua programu hiyo kwanza kabla ujapakua soko hilo.
- Huawei Mobile Services