Ni wiki nyingine tena tunakutana kwenye Habari kubwa za wiki. hapa tukikuletea muhtasari wa yale yote yaliyojiri kwenye ulimwengu mzima wa teknolojia kwa wiki nzima kwenye tovuti ya Tanzania Tech, Basi bila kupiteza muda twende tukaangalie habari hizo.
Wiki hii habari kubwa kuliko zote ilikuwa ni uzinduzi wa simu mpya kutoka kampuni ya Tecno, simu hizo mpya zimezinduliwa huko nchini Nigeria wiki hii. Simu hizo tofauti na watu ambavyo walidhani simu hizi zinakuja na sifa za kawaida pamoja na muonekano mpya wa kioo yaani Full Display. Kwa upande wa simu za Tecno F simu hizi zinakuja kwaajili ya watu wanaotaka simu za bei nafuu napia ni simu za kwanza kutoka kampuni ya tecno kutumia mfumo wa Android Go.
Wiki hii habari nyingine kubwa ilikuwa inahusu mtandao wa YouTube, wiki hii makao makuu ya mtandao huo yalivamiwa na mwanamke aliyekuwa na lengo la kulipiza kisasa, na ripoti zinadai kuwa mwanamke huyo alikuwa akidhani kuwa anabaguliwa na matandao huo na inasemekana ndio chanzo cha yeye kuvamia makao makuu ya mtandao huo na kujeruhi watu wanne na baadae kujipiga risasi akiwa ndani ya jengo hilo.
Wiki hii pia whatsapp imeingia kwenye vichwa vya habari kwa kutangaza kuja na njia mpya ya kubadilisha namba, njia hii itakuwezesha kubadilisha namba na kutumia ujumbe kwa watumiaji pale tukapo badilisha namba njia hii itakuwa muhimu kusaidia watu hasa wale wanao tumia WhatsApp ya biashara.
Wiki hii pia Samsung ilizindua laptop zake mpya, Laptop hizi za sasa zinasemekana kuja zikiwa zimeboreshwa zaidi pamoja na sifa mpya huku zikiwa na muonekano wa kisasa zaidi. Habari kutoka kwenye tovuti ya Samsung zinasema laptop ya Notebook 3 inakuja kwa aina mbili yaani laptop yenye kioo cha inch 14 na nyingine ikiwa na nchi 15.
Ripoti kutoka kwenye tovuti ya Swahili Times zinasema, Vodacom wametoa tamko na kusema kuwa itaendelea kutoa huduma za umeme kama kawaida lakini Kutakuwa na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%) anayotozwa mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa.
Roboti sophia kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuja Afrika kwenye mkutano wa Egypt’s Creative Industry Summit unaotegemewa kufanyika kuanzia tarehe 17 mwezi huu wa nne mpaka tarehe 18 huko nchini Misri.
Kifaa hicho kime tengenezwa na wataalamu kutoka chuo cha MIT huko nchini marekani, na inasemekana kifaa hicho kwa sasa kinao uwezo maalum kusikia mawazo yako na kuyapeleka moja kwa moja kwenye kompyuta. Kwa maana nyingine ni kwamba, kwa sasa kifaa hicho kinasaidia mtu kufanya mambo mbalimbali kwenye kompyuta au vifaa mbalimbali ya kieletroniki kwa kutumia au kwa kusikiliza mawazo yako.
Na hizo ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii nzima, kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita unaweza kusoma habari hizo hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, mpaka wiki ijayo nakutakia jumapili njema.
Habari jamani naulizia kulikuwa na Apu ya kudanlodi movie inaitwa Theater plus sasahivi haipatikani .kulikoni.