Gamshoe Kiatu Kilicho Tengenezwa kwa Kutumia Pipi za Kutafuna

Kiatu hichi kimetengenezwa kwa asilimia 20 ya pipi za kutafuna zilizo tumika
Gamshoe Kiatu Kilicho Tengenezwa kwa Kutumia Pipi za Kutafuna Gamshoe Kiatu Kilicho Tengenezwa kwa Kutumia Pipi za Kutafuna

Ni wazi kuwa ni watu wengi sana hutumia pipi za kutafuna (chewing gum) kutokana na umati huu wa watu kutumia pipi hizo kumekuwa na tatizo kubwa duniani la kutupa pipi hizo ovyo pale zinapo malizika kutumika.

Sasa huko Amsterdam nchini Uholanzi wao wamefanikiwa kupata suluhisho la tatizo hilo kwa kutengeneza kiatu cha kwanza kabisa kilicho tengenezwa kwa mabaki ya pipi hizo za kutafuna.

https://youtu.be/f155BH2MErE

Advertisement

Kwa ushirikiano wa shirika la masoko ya jiji Iamsterdam, kampuni ya ubunifu wa nguo na viatu ya Explicit Wear na kampuni ambayo inafanya kazi ya kurudisha kwenye matumizi pipi za kutafuna zilizo tumika ya Gumdrop, kwa pamoja wamekuja na aina hii ya kiatu ambacho kimepewa jina la Gamshoe ambacho kime tengenezwa kwa asilimia 20 ya pipi hizo za kutafuna zilizo tumika.

Kwa mujibu wa tovuti ya amsterdam, soli ya kiatu hicho ndio imetengenezwa kwa aina hiyo ya malighafi ambayo imepewa jina la Gum-Tec. Gum-Tec ni aina ya malighafi inayo tengenezwa na kampuni ya Gumdrop ambayo yenyewe inapatikana kutoka kwenye pipi za kutafuna zilizotumika, sasa kampuni hiyo inasema kuwa asilimia 20 ya malighafi hiyo ni pipi za kutafuna zilizotumika.

Anna Bullus ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Gamdrop amesema kuwa, waligundua kuwa pipi za kutafuna zimetengenezwa na kiasi flani cha mpira na kupitia utafiti wao waliweza kufanya mabadiliko ya aina hiyo ya mpira na kutengeneza aina nyingine ya mpira ambayo ndio iliyo tumika kutengeneza soli ya kiatu hichi cha Gamshoe.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alisema, kiatu hicho kimetengenezwa kwa ngozi ngumu kwa juu na kwa chini ndio kimetengenezwa kwa malighafi hiyo inayo tokana na pipi za kutafuna ambapo inasemekana kuwa hata baada ya utengenezaji wake ukinusa soli ya kiatu hicho bado inanukia kama pipi za kutafuna.

Kiatu hicho cha Gumshoe kinatarajiwa kuingia sokoni mwezi wa sita huku kikiwa kinauzwa kwa dollar za marekani $232 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 532,000, kwa mujibu wa viwango vya kubalisha fedha vya siku ya leo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use