Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Bei na Sifa za Tecno F1,Tecno F2 na Tecno POP 1

Kama wewe ni mpenzi wa simu za tecno hizi hapa sifa za simu mpya
Sifa za Tecno F Sifa za Tecno F

Kama uliangalia uzinduzi wa Simu za Tecno jana lazima ulifanikiwa kuona Tecno ikizindua simu zake mpya za Tecno Camon X, Tecno Camon X Pro pamoja na simu zake za bei rahisi za Tecno F1 Tecno F2 na Tecno POP 1 au Tecno F3 simu ambazo ndio za kwanza kutoka kampuni ya Tecno zinazokuja na mfumo wa Android Go.

Inawezekana Labda ukufanikiwa kuangalia uzinduzi huo hivyo basi kama unataka kujua sifa za Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon X Pro unaweza kusoma kwenye makala zetu zilizopita, lakini hapa tutaenda kuangalia sifa za Tecno F1 na Sifa za Tecno F2 pamoja na Sifa za Tecno POP 1 au Tecno F3, Basi bila kupoteza muda Twende tukangalie sifa hizo.

Advertisement

Sifa za Tecno F1 na Tecno F2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya FullView display capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1440 x 720 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo: Go Edition)
  • Uwezo wa Processor – 1.3GHz quad-Core MT6735 CPU
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720 GPU
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 .yenye uwezo wa kuongezewa kwa Memory Card hadi ya GB 128
  • Ukubwa wa RAM – GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 2
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 (Samsung lens) yenye LED flash, f/2.2 aperture
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3000mAh built-in battery
  • Viunganishi – 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth 4.2, GPS + GLONASS
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Black, Gold
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Nano SIM, Inayo Radio FM
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4

Simu hizi za Tecno F1 na Tecno F2 zina tegemewa kuingia sokoni wiki ijayo na inatarajiwa zitakuja kwa bei nafuu ya Tsh 200,000 hadi Tsh 250,000 au chini ya hapo. Hata hivyo simu za Tecno F1 na Tecno F2 hazija tofautiana kisifa.

Sifa za Tecno (POP 1) F3

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya FullView display capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1440 x 720 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo: Go Edition)
  • Uwezo wa Processor – 1.3GHz quad-Core MT6735 CPU
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720 GPU
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 .yenye uwezo wa kuongezewa kwa Memory Card hadi ya GB 128
  • Ukubwa wa RAM – GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 rear camera with LED flash, f/2.2 aperture
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3000mAh built-in battery
  • Viunganishi – 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth 4.2, GPS + GLONASS
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Black, Gold
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Nano SIM, Inayo Radio FM
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4

Tofauti kubwa iliyoko kwenye Tecno POP 1 au Tecno F3 ni kwa upande wa kamera ya mbele ambayo yenyewe itakuwa na kamera ya Megapixel 5. Simu hii ya Tecno POP 1 au F3 itakuja kwa bei nafuu ya kuanzia Tsh 200,000 hadi Tsh 280,000 au chini ya hapo. Simu zote hizi zinaweza kuanza kupatikana kuanzia wiki ijayo.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use