Linapokuja swala la Apps nzuri ni wazo kuwa kila mtu anajua apps au programu ambazo ni nzuri kwake kwa namna moja ama nyingine, Lakini hapa Tanzania Tech tunakuletea list ya apps ambazo tunajua zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kwenye matumizi ya simu yako ya kila siku, basi bila kupoteza muda twende tukangalie App hizi nzuri za Android.
1. GlassWire Data Usage Monitor
GlassWire Data Usage Monitor ni App nzuri ambayo itakusaidia kuweza kudhibiti data au internet kwenye simu yako, sasa najua kuna programu nyingi zenye kuweza kufanya hivi lakini utofauti wa App hii upo kwenyeuwezo wake wa kutoa taarifa pale kiasi flani cha MB au GB kinapofika. Yaani kwa kutumia App hii utaweza kuseti kiasi flani cha MB kikifika basi upate ujumbe maalum kukutaka kujua MB au GB zako zimefikia kiwango hicho, Vilevile unaweza kuangalia kiasi cha data kwa kila App.
2. Notisave – save notifications
Notisave hii ni app nzuri ambayo itakusaidia wewe kuweza kuhifadhi Notification zako kwaajili ya kuzisoma baadae. Yaani app hii itakusaidia kuepukana na notification nyingi juu ya kioo cha simu yako na notification hizo zitahifadhiwa ndani ya App hiyo na utaweza kuzisoma baadae pale unapokua na nafasi. Kwa mfano kama umefollow akaunti mbalimbali kwenye youtube na kila mara unapata notification au taarifa za video mpya unaweza kujikuta kioo cha simu yako kimejaa taarifa hizo, ndipo App hii ya Notisave inapokuwa na umuhimu, ijaribu sasa.
3. Circle SideBar
Circle SideBar hii ni App nzuri ambayo itakusaidia wewe kuweza kutumia app zako kwa haraka. Kwa kutumia App hii utaweza kuongeza sehemu mpya pembeni ya kioo chako ambayo itakusaidia wewe kuweza kufungua programu mbalimbali kwa haraka. Sehemu hii ni kama ile ya kwenye Galaxy S7 na S6 Edge ambapo unaweza kupapasa kidole kwa pembeni ya kioo chako na utaweza kufungua programu mbalimbali. App hii ni nzuri pale unapokuwa labda unachati uku unafanya mambo mengine kwenye simu yako.
4. Mirror Emoji Keyboard & Stickers For Text Messages
Mirror Emoji Keyboard hii ni App nzuri itakayo kusaidia wewe kuweza kutengeneza Emoji zenye sura yako na utaweza kuwatumia Emoji hizo watu mbalimbali. Unachotakiwa kufanya ni kupiga picha ya selfie kwa kutumia App hii na itaweza kutengeneza emoji ya sura yako kwa haraka sana. Tofauti ya App hii na App nyingine zenye uwezo wa kufanya hivi ni kuwa app hii inakupa uwezo wa kutengeneza emoji nzuri sana na zinazo fanana na wewe kwa kiasi flani.
5. Free music for YouTube: Stream
Free music for YouTube hii ni App nzuri ya Android inayokuwezesha kusikiliza na kuangalia video za muziki unazozipenda kwa haraka zaidi. App hii tofauti na App ya YouTube app hii inazo video za muziki pekee naunaweza kuchagua ni muziki wa aina gani unapenda kama vile rap, r&b na aina nyingine nyingi za muziki. Mbali na hayo app hii itakuwezesha kuangalia video hizo hata ukuwa unafanya mambo mengine kwenye simu yako, yaani utakuwa na uwezo wa kuangalia video za muziki unao upenda kwa pembeni uku unafanya mambo mengine kwenye simu yako.
Na hizo ndio App nzuri ambazo nimekuandalia siku ya leo, kama unataka kujua app nyingine nzuri za Android unaweza kusoma list nyingine ya App nzuri hapa. Kama unayo au unajua apps nyingine nzuri za Android tuambie kwenye maoni hapo chini na tutaziweka kwenye list hii aul list nyingine ya App nzuri za Android.
Nawakubali saana hongera ongezeni zingine tena wapendwa
Karibu sana.
mjaribu kukimbizana na kasi ya technolojia kwa ubunifu zaidi
Asante sana Godias, Kama una ushauri wowote unaweza kutuandikia hapa au kwa kutumia sehemu ya wasiliana nasi hapo chini, Asante.
Ninatumia Samsung galaxy Lakin storage yke ni ndogo, nimeweka sd card, lakin nashindwa kudownliad app playsotere moja kwa moja hadi kweny sd card, inakataa, je nifanye nini ili kukabiliana na hilo, coz kuna apps nying nahtaj but inakataa storage..? msaada
Ni Samsung Galaxy ipi kaka.
nimezipendaaa
Karibi