Zanzibar Kujenga Kiwanda cha Kutengeneza Simu za Mkononi

Kiwanda hicho kuanza uzalishaji wa simu kamili baada ya miaka minne
zanzibar kutengeneza simu za mkononi zanzibar kutengeneza simu za mkononi
<a href="https://www.gettyimages.com/" rel="nofollow" target="_blank"><span style="font-size: x-small;">Photo by Getty Images</span></a>

Habari kupitia gazeti la kila siku la Habari leo zinasema kuwa, Zanzibar inatarajia kujenga kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza simu za mkononi na kutoa ajira kwa wananchi wa visiwa hivyo. Habari hizo zinaendelea kusema, kiwanda hicho kitakacho anzishwa hivi karibuni na Kampuni ya U$I kutoka Korea Kusini, kitaanza kwa kuunganisha vifaa vya simu na kisha baada ya miaka minne kuanza kutengeneza simu za mkononi.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud alisema kuwa wiki mbili zilizopita, wamesaini makubaliano na kiwanda cha simu za mkononi na tayari wawekezaji hao wamepewa eneo katika eneo la viwanda vidogo. “Kwa sasa wanamalizia taratibu na wamesema katika miezi miwili hadi mitatu watakuwa wameanza kazi ya kuunganisha simu kutoka Korea Kusini, na sasa badala ya kununua kutoka Korea sasa simu za mkononi zitakamilika hapa na kwenda kuuzwa maeneo mengine,” alisema.

Mkuu wa mkua huyo aliendela kusema kuwa, kiwanda hicho anachodhani hakuna katika nchi za Afrika Mashariki, kitaanza kwa kuajiri watu 60 hadi 120 kwa kuanzia na baada ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji wa simu kamili ambao unadhaniwa kuwa baada ya miaka minne, basi muda huo watatoa fursa kwa vijana 10 zaidi kutoka Zanzibar kupata mafunzo ya ziada katika maeneo ya uzalishaji simu na kupata shahada za uzamili na uzamivu kwenye teknolojia hiyo, hivyo kuwawezesha kufanya kuzalisha simu za mkononi kutoka mkoa huo.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use