Huu Ndio Ubora na Ugumu wa Simu Mpya ya Galaxy S9

Kama unataka kununua simu mpya ya Galaxy S9 basi angalia video hii
Ugumu wa Samsung Galaxy S9 Ugumu wa Samsung Galaxy S9

Hivi karibuni Samsung imezindua simu zake mpya za Samsung Galaxy S9 pamoja na Galaxy S9 Plus, Simu hizi zinaonekana tayari zimesha ingia sokoni nchini marekani na sasa ni wakati wa kuangalia ubora na ugumu wa simu hizo.

Kama bado hujajua JerryRigEverything ni jina la channel ya Youtube ya jamaa anae tambulika kwa jina moja la Zack, jamaa huyu hufanya majaribio ya simu mbalimbali kwa kuzikunja, kuzisugua na vifaa maalum na hata kuzichoma simu kwenye kioo ili kuangalia ugumu na ubora wa simu hizo.

Sasa wiki hii jamaa huyo amefanya majaribio ya simu mpya ya Galaxy S9 na kwa sababu wote tunajua wengi wengependa kujua, nimeona nikusogezee hii ili uweze kujua kama Galaxy S9 ni simu bora kwako kununua mwaka huu 2018 ama lah!..

Advertisement

Vipi unaonaje ugumu na ubora wa simu hii mpya ya Samsung Galaxy S9..? unadhani kweli inafaa wewe kununua kutokana na kufaulu majaribio hapo juu..? tuambie kwenye moani hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use