Mtandao wa Spotify Wafunguliwa Rasmi Nchini Afrika Kusini

Mtandao huo umeingia Afrika kwa mara ya kwanza Kabisa
spotify Afrika ya kusini spotify Afrika ya kusini

Mtandao maarufu wa kusikiliza na kusambaza muziki wa Sporify umefungua huduma zake Afrika kwa mara ya kwanza, huku ikianza na nchi ya Afrika Kusini. Mtandao wa Spotify ulianzishwa mwaka 2008 na ulianza kwa kufunguliwa kwa nchi za ulaya na sasa unafikia zaidi ya nchi 60 duniani.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao Spotify kwa Afrika Mashariki na Kati Claudius Boller aliiambia Reuters kuwa “Tunaamini Afrika Kusini ni nchi nzuri ya kuanza, Tuliangalia eneo la teknolojia, tuliangalia ukomavu na kwa kweli Afrika Kusini inaonekana duniani kote kama soko muhimu la muziki.”

Advertisement

Kwa sasa bado haijajulikana lini mtandao huo utasogea kwa nchi zingine za Afrika, huku mkurugenzi huyo akisisitiza kuwa Afrika kusini ni hatua ya kwanza hivyo pengine huduma hizo zitakuja kwa nchi nyingine za Afrika ikiwemo na Tanzania.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use