Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Bora za Infinix Bei Zake na Mahali Pakununua (2019)

Unatafuta simu bora ya kununua kutoka kampuni ya Infinix..? soma hapa
Simu bora za Infinix (2018) Simu bora za Infinix (2018)

Kama bado ulikua hujui infinix ni jina la kampuni ya simu ambayo makao yake makuu yako huko Hong Kong, kampuni hii ilianzishwa mwaka 2012. Kampuni hiyo ina vituo vya utafiti na maendeleo huko Paris na Shanghai. Lakini Simu za mkononi za Infinix zinatengenezwa nchini China na baadae kusambazwa Afrika na nchi zingine kama india na jirani.

Sasa simu za Infinix zimekuwa kwenye soko la Afrika kwa muda mrefu sana, lakini kama ilivyo simu za tecno simu hizi pia zinawatumiaji wengi sana kwenye nchi za Afrika hii inatokana na urahisi wa Bei zake pamoja na uwezo wa simu hizi kukudhi haja za watumiaji wengi barani hapa.

Advertisement

Sasa basi, kuliona hili leo nimeona nije na list ya simu hizi bora za Infinix ambazo najua zainaweza zikawa bora kwa namna moja ama nyingine hii ikitegemeana pia na mahitaji yako kwenye simu janja. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii, kumbuka list hii haijapagwa kwa namba hivyo hii sio kumi bora.

1. Infinix Zero 5

Infinix Zero 5 ni moja kati ya simu nzuri sana kutoka kampuni ya Infinix, simu hii ilizinduliwa huko dubai na ndio simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo kuja na mfumo wa kamera mbili kwa nyuma sifa nyingine za Infinix Zero 5 ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Zero 5

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.98″ 1920 by 1080 FHD IPS capacitive touchscreen.
  • 16 MP front-facing camera with LED flash
  • 12MP +13MP dual back cameras with LED flash.
  • OS: Android 7.0 Nougat with XOS v3.0
  • 64GB or 128GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 2TB)
  • Octa-core 2.60 GHz with Helio P25 chipset
  • 6GB of RAM
  • 4350mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 654,000

Nunua Infinix Zero 5

2. Infinix Zero 4 Plus

Infinix Zero 4 Plus ni simu nyingine bomba kutoka kampuni ya Infinix, simu hii ni toleo la juu la simu ya Infinix Zero 4, simu hii kwa muundo inafanana na na toleo la Infinix Zero 4 ambapo simu hii inakuja na kioo kikubwa pamoja na sifa zingine.

Sifa za Infinix Zero 4 Plus

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.98″ 1920 by 1080 FHD IPS capacitive touchscreen.
  • 13 MP front-facing camera LED flash
  • 20.7MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow upgradable to Android 7.0 Nougat
  • 32GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Deca-Core 2.1 GHz with Helio X20 (MT6797M) processor, 4GB of RAM
  • 4000mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 900,000

Bado Haipo Mtandaoni

3. Infinix Zero 4

Infinix Zero 4 hii ndio simu ambayo ndio ndogo ya simu ya Infinix Zero 4 Plus au kwa jina lingine Infinix Zero 4 Pro ambapo simu hii inakuja na sifa za msingi kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Zero 4

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.5″ 1920 by 1080 FHD IPS capacitive touchscreen.
  • 8 MP front-facing camera LED flash
  • 16 MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow upgradable to Android 7.0 Nougat
  • 32GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-Core 1.3 GHz with MediaTek MT6753 processor, 3GB of RAM
  • 3200mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 750,000

Bado Haipo Mtandaoni

4. Infinix Hot S3

Infinix Hot S3 ni simu ambayo ndio simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Infinix kuwa na kioo chenye ratio ya 18:9, Simu hii inakuja na uwezo mzuri sana pamoja na mfumo mpya wa Android Oreo 8.0 na sifa zingine kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot S3

  • OS: Android 8.0 Nougat with XOS v3.0
  • SIM Type: Dual SIM (Nano)
  • 4G LTE: YES, LTE
  • Screen Size : 5.65 Inches HD IPS Touchscreen
  • Screen Resolution: 720 x 1440 pixels (~285 PPI)
  • Processor Type: Octa-core 1.40 GHz, Snapdragon 430 chipset
  • RAM: 3GB
  • Internal Storage: 32GB
  • External Storage: microSD, up to 128GB
  • Back / Rear Camera: 13MP camera & LED Flash
  • Front Camera: 20MP with LED flash
  • Battery: 4000 mAh (non-removable)

BEI – Tsh 350,000

Bado Haiko Mtandaoni

5. Infinix Note 3 Pro

Infinix Note 3 Pro ni simu nyingine ya Infinix ambayo ni toleo kubwa la simu ya Infinix Note 3, simu hii inakuja na RAM kubwa zaidi ya Infinix Note 3 kwa upande mwingine Infinix Note 3 na Infinix Note 3 Pro hazinatofauti kubwa sana zaidi ya uwezo wa RAM.

Sifa za Infinix Note 3 Pro

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 6.0″ 1920 by 1080 FHD IPS capacitive touchscreen.
  • 5MP front-facing camera LED flash
  • 13MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow
  • 4G LTE support
  • 16GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-core 1.3GHz processor, 3GB of RAM
  • 4500mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 450,000

Bado Haipo Mtandaoni

6. Infinix Note 3

Hii ndio simu ndogo ya Infinix Note 3 Pro, kama nilivyo tangulia kusema awali simu hii hainatofauti kubwa sana na Infinix Note 3 Pro lakini kwa faida yako hizi hapa sifa zingine za simu hii.

Sifa za Infinix Note 3

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 6.0″ 1920 by 1080 FHD IPS capacitive touchscreen.
  • 5MP front-facing camera LED flash
  • 13MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow
  • 16GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-core 1.3GHz processor, 2GB of RAM
  • 4500mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 350,000

Bado Haipo Mtandaoni

7. Infinix Zero 3

Infinix Zero 3 ni simu nyingine kutoka kampuni ya Infinix Zero 3 ni simu nyingine kutoka kampuni ya infinix Zero 3 ni simu kubwa ya infinix Zero 2 simu hii inauwezo karibiana na Zero 2 lakini zero 3 yenyewe inayo kioo kikubwa pamoja na kamera kubwa zaidi, sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Zero 3

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.5″ 1280 by 1920 HD capacitive touchscreen, 401 PPI
  • Quad-core 2.2GHz processor, 3GB of RAM
  • 16/32GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 2TB)
  • OS: Android 5.1 Lollipop
  • 20.7MP back camera with LED flash.
  • 5MP front-facing camera with LED flash
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB
  • 3,300mAh battery capacity.

BEI – Tsh 300,000

Bado Haipo Mtandaoni

8. Infinix S2 Pro

Infinix S2 Pro ni simu ambayo ni kubwa ya simu ya Infinix S2, simu hii tofauti yake kubwa ni kuwa simu hii inakuja na uwezo mkubwa wa RAM na uwezo mkubwa wa ukubwa wa ndani na vilevile simu hii inakuja na kamera mbili kwa mbele pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Infinix S2 Pro

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.2″ 720 by 1280 HD IPS capacitive touchscreen.
  • 8MP + 13 MP front-facing camera LED flash
  • 13MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow upgradable to Android 7.0 Nougat
  • 32GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-core 1.3GHz processor, 3GB of RAM
  • 3000mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 450,000

Nunua Hapa Infinix S2 Pro

9. Infinix S2

Infinix S2 ndio simu ndogo ya Infinix S2 Pro simu hii inakuja na utofauti kidogo na Infinix S2 Pro kwani simu hii inakuja na bei nafuu pamoja na sifa ndogo kidogo ya simu ya Infinix S2 Pro, sifa za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix S2

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.2″ 720 by 1280 HD IPS capacitive touchscreen.
  • 8MP + 13 MP front-facing camera LED flash
  • 13MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow upgradable to Android 7.0 Nougat
  • 16GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-core 1.3GHz processor, 2GB of RAM
  • 3000mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 350,000

Bado Haipo Mtandaoni

10. Infinix Hot S

Infinix Hot S ni simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Infinix kuwa na fingerprint na pia ndio simu ya kwanza kabisa kwa mfululizo wa matoleo ya Infinix Hot S. Simu hii inakuja na Ram ya GB 3 pamoja na sifa zingine kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot S

  • Dual-SIM dual-standby capability
  • 5.2″ 1920 by 1080 IPS capacitive touchscreen.
  • 8MP front-facing camera LED flash
  • 13MP back camera with LED flash.
  • OS: Android 6.0 marshmallow with XUI
  • 16 or 32GB of built-in storage expandable via microSD card (up to 128GB)
  • Octa-core 1.5GHz processor, 3GB/2GB of RAM
  • 3,000mAh battery capacity.
  • Wi-Fi, hotspot, Wi-Fi direct; Bluetooth 4.1; GPS/GLONASS; microUSB

BEI – Tsh 300,000

Bado Haipo Mtandaoni

11. Infinix Hot 5 Pro

Infinix Hot 5 Pro ni simu nyingine kutoka kampuni ya Infinix, simu hii zinakuja za aina mbili yaani Infinix Hot 5 Pro pamoja na Infinix Hot 5 simu hizo hazina tofauti sana na karibia zinafanana wakati simu ya Infinix Hot 5 Pro ikija na sifa kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot 5 Pro

  • OS: Android 7.0 Nougat
  • Screen Size: 5.5-inch IPS HD display
  • Design Dimension:156.6 x 76.2 x 8.8mm
  • SIM Type: Dual SIM
  • 3G
  • Processor: Quad-core MediaTek
  • RAM: 2GB
  • ROM: 32GB – 16GB
  • Back Cameral: 8MP back camera
  • Front: 5MP front camera
  • Battery: 4000mAH

BEI – Tsh 400,000

Bado Haipo Mtandaoni

Updated (imeongezewa) 25-08-2018

12. Infinix Note 5 na Note 5 Pro

Simu nyingine nzuri sana ya Infinix ambayo utaweza kununua kwa sasa ni simu hizi za Infinix Note 5 na Note 5 Pro. Simu hizi ni nzuri sana na kama umekuwa ukitaka simu nzuri kwa bei nafuu simu hii ni moja kati ya simu ambayo pengine unahitaji kuiangalia kwa ukaribu. Simu hii inakuja na mfumo wa Android 8.1 ambao huu ni mfumo wa Android One, mfumo huu ndio mfumo unaotumika kwenye simu kama Google Pixel na nyingine nyingi hivyo ni wazi utaweza kufurahia simu hii hasa kwenye mfumo wa AI kwa mfumo huu unakuja moja kwa moja kutoka kampuni ya Google.

Sifa za Infinix Note 5

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS FHD LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 X 2160 pixels, 18:9 ratio (~407 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz, MediaTek Helio P23 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali G71 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3 kwa Note 5 na GB 4 kwa Note 5 Pro
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 12 yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, microUSB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Milan Black, Berlin Gray na Ice Blue colors..
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Bei – Tsh 450,000 – 500,000

NUNUA HAPA KWA TSH 500,000

13. Infinix Hot S3X

Kama kwa muda mrefu umekuwa ukitamani kushika iPhone X basi hili ni suluhisho kwako. Infinix Hot S3X ni toleo la maboresho la simu ya Hot S3 lakini toleo hili lina maboresho makubwa sana, Simu hii ndio simu ya kwanza kutoka kampuni ya Infinix yenye ukingo wa juu pia simu hii inakuja na mfumo wa AI kwenye kamera zake. Simu hii inatumia processor za kisasa za Snapdragon ambazo ni processor zenye viwango ukilinganisha na processor walizokuwa wanatumia awali za Mediatek.

Sifa za Infinix Hot S3X

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~268 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – 1.4GHz Octa-Core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 430 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 505.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 3 na nyingine ina RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine inakuja na Megapixel 2 zenye Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue, na Gray
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, G-sensor, E-compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor, Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID)

Bei – Tsh 350,000 – 400,000

Bado Haipo Mtandaoni

14. Infinix Zero 6 Pro

zero 6 pro

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Infinix na ungependa kuwa na simu yenye muonekani mzuri lakini pia yenye sifa bora basi Infinix Zero 6 Pro ni simu bora sana kuwa nayo. Simu hii inakuja na sifa nzuri sana pengine kuliko simu zote kwenye list hii, pia simu hii inakuja na muonekano mpya wa kisasa wenye kufanya simu hii iwe moja kati ya simu bora kabisa kutoka kampuni ya Infinix.

Sifa za Infinix Zero 6 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 2160×1080 Pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 636 (SDM636).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 MP, Low-light Sensor na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye 2PD. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Quad LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3650 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Milan Black na Sapphire Cyan.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

BEI – Tsh 700,000 – 760,000

15. Infinix Hot 7

Simu Bora za Infinix Bei Zake na Mahali Pakununua (2019)

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Infinix basi ni vyema sana kuifahamu simu mpya ya Infinix Hot 7, simu hii inakuja na sifa bora sana lakini inapatikana kwa bei nafuu sana. Mbali ya unafuu wake moja kati ya vitu ambayo utafurahia zaidi kwenye simu hii ni pamoja na battery ambayo inakuja na uwezo wa 4000 mAh ambayo inaweza kudumu na chaji kwa siku nzima kutokana na matumizi yako.

Sifa za Infinix Hot 7

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1550 x 720 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6580P Chipset.
  • Uwezo wa Processor (CPU) – Quad-core 1.3 GHz 4x Cortex MT 6580
  • Uwezo wa GPU – Bado haijajulikana
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 16 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2 au GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8, yenye LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 13 huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Purple.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Aina za Sensor – Fingerprint scanner; Face recognition; Gyroscope; Proximity; e-Compass; Light; G-sensor.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

BEI – Tsh 380,000 – 350,000

Na hizo ndio simu za Infinix ambazo unaweza kununua kwa sasa, Kumbuka bei ya simu hizi inaweza kuongezeka au kupungua zaidi ya bei zilizo onyeshwa hapa. Pia unaweza kupata simu hizi kupitia maduka mbalimbali na kwa dar es salaam unaweza kuzipata simu hizi kupitia maduka ya simu mbalimbali kariakoo. Hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu kila siku tutakuwa tukiweka link za simu hizi pale tutakapo zipata kupitia kwenye soko la mtandaoni la Jumia.

28 comments
  1. Kama nipo mkoan na nnahitaji sm mojawap kat ya hz nafanyaje kuzipata? Na kma ujuavy mikoani sm bei ni juu sana. Na je naruhusiwa kulipa hela kidogokidogo na nikimaliza napt hy bidhaa?

  2. Aisee mko vzur sana…natumia infx not5 kwa sasa iko pw sana Imesha maliza mwaka 1.5 Nahaija wai kisumbua…kabisa ila kwa sasa Naitaji zero6..

  3. Maoni*Naomba kuuliza,nikihitaji simu zenu mnitengenezee kwa nembo yangu mf,nina wateja 400.000/=nataka tutumie simu za nembo ya kampuni,inawezekana?
    Swali la pili:ni nini vigezo vya kuwa wakala wenu?

  4. Hongera sana kwa kuwa na simu bora mm ninayo infinix hot 5 namaliza mwaka na miezi 3 hajasumbua ila nahitaji nibadilishe nunue toleo lingine je nawapata wapi

  5. maoni yangu hizi simu ziangariwe vizuri kwanini ukiwa upo kwenye kuchat simu ikapigwa huwezi ona pakupokelea mpaka ikatike ndio ukute miiss coll

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use