in

Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Huawei Porsche Mate RS (2018)

Simu hii inakuja na Fingerprint mbili mbele kwenye kioo na nyuma

Sifa za Huawei Porsche Mate RS (2018)

Kila mwaka Huawei huzindua toleo la simu zake za Huawei Porsche na toleo hili huwa maalum kwaajili ya watu maalum au watu wenye uwezo wa juu, Sasa mwaka huu kwenye uzinduzi wa Huawei P20 na P20 Pro, Huawei ilitangaza toleo jipya la Huawei Porsche Mate RS (2018), simu hii inakuja na sifa mpya nyingi sana ukitofautisha na Huawei Porsche ya mwaka jana.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa muonekano simu hii ni nzuri sana na inakuja na uwezo wa tofauti ambapo simu hii inakuja na mfumo wa AI ambao pia unapatikana kwenye simu za Huawei P20 na P20 Pro. Lakini kinachofanya simu hii kuwa maalum kwa watu maalum ni sifa za simu hii, kwa ufupi hizi hapa ndio sifa za Huawei Porsche Mate RS (2018).

Sifa za Huawei Mate RS (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya AMOLED , chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1440 x 2880 pixels, 18:9 ratio (~538 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko kwa machaguo mawili GB 256 pamoja na GB 512. Haina sehemu ya memory card.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko tatu moja ikiwa na Megapixel 40 yenye (f/1.8, 1/1.7″, OIS) na Kamera nyingine inayo Megapixel 20 yenye (f/1.6, 27mm) na ya mwisho inayo Megapixel 8 ikiwa na teknolojia za (f/2.4), Leica optics, 3x optical zoom, phase detection, laser autofocus pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 4000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Red
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Haingizi maji wala vumbi.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint mbili kwa mbele kwenye kioo na nyingine iko kwa nyuma

Simu hii inatarajiwa kuingia sokoni mwezi wa nne tarehe 12 na kwa upande wa bei, hapa natumaini umekaa chini maana hii bei sio mchezo.. Simu hii ya Huawei Porsche Mate RS (2018) inategemewa kuingia sokoni ikiwa inauzwa Euro €1,695 kwa simu ya GB 256 ambayo ni sawa na Tsh 4,747,000 na Euro €2095 kwa simu yenye GB 512 ambayo ni sawa na Tsh 5,866,000.

Ukweli ni kwamba naomba usisubiri simu hii ya Huawei Porsche Mate RS (2018) maana haitoweza kufika hapa Tanzania na hii ni kitokana na bei yake maana Tsh 5,866,000 ukijumlisha na kodi kwa makadirio inaweza kufika hadi Tsh 7,000,000. Kumbuka Bei hizo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivyo bei inaweza kuongezeka zaidi.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Huawei Porsche Mate RS (2018)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments