Samsung Kuzindua Aina Mpya ya TV za QLED Hapo Kesho

Jandae na TV mpya za QLED kutoka Samsung mwaka huu 2018
Samsung Kuzindua Aina Mpya ya TV za QLED Hapo Kesho Samsung Kuzindua Aina Mpya ya TV za QLED Hapo Kesho

Wakati kwa sasa watu wengi hapa Tanzania wakiwa wanatumia TV za OLED pamoja na LED Samsung imeanza kujiandaa kuingiza sokoni aina mpya ya TV zake za mwaka 2018 zenye teknolojia ya QLED hapo kesho, March 7, 2018.

Tamasha la uzinduzi wa TV hizo mpya kwa mwaka huu 2018 litafanyika huko nchini marekani kwenye jengo maarufu la American Stock Exchange ambalo liko huko Manhattan, ambapo kampuni ya Samsung inategemewa kuja na aina mbalimbali za TV zenye teknolojia ya hiyo ya QLED.

Advertisement

Sasa kabla ujauliza najua unataka kujua nini maana ya QLED na kuna utofauti gani na kati ya TV za QLED na TV za LED au OLED, sasa kukujibu maswali yako kwa urahisi unaweza kuangalia Video hapo chini.

Kurahisisha hapa utofauati mkubwa ulioko kwenye TV hizi mbili ni rangi pamoja na uwezo wa kuonyesha mwanga. QLED ni aina ya teknolojia ya TV kutoka samsung ambayo inategemea mwanga maalum ili kuweza kuonyesha rangi nzuri hii ikiwa imetengenezwa kisasa zaidi na kampuni ya Samsung ikiwa pamoja na kuekewa uwezo wa hali ya juu wa kuonyesha rangi zaidi.

Kwa upande wa OLED hizi ni TV ambazo hazi itaji mwanga maalum ili kuonyesha picha nzuri bali, TV hizi hutoa mwanga wake kwenye Pixel zake yenyewe hivyo kufanya rangi kuwa angavu na kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nzuri zaidi hasa rangi nyeusi. Sasa utofauti ambao ni mkubwa sana kwenye TV hizi mbili ni mwanga, rangi pamoja na aina ya teknolojia na hii ni kutokana na kuwa QLED ni teknolojia kutoka kampuni ya Samsung. Yaani hii ni kama sehemu ya kutangaza TV kutoka kampuni ya Samsung.

Sasa kama unataka kujua zaidi kuhusu tofauti ya TV zenye teknolojia ya LED pamoja na TV zenye teknolojia ya OLED unaweza kusoma hapa, pia endapo unataka kujua ni hatua gani za kufuata wakati unataka kununua TV unaweza kusoma makala hapa.

1 comments
  1. Maoni* mimi hamis ally kuludishiwa mafaili pamoja sim yangu sikuhizi haoneshi video sim yangu nokia 310

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use