Ripoti asubuhi ya leo zinasema huenda kampuni ya Huawei ikawa inajiandaa kuja na simu yake mpya yenye ukubwa wa ndani wa GB 512, habari kutoka tovuti ya Android Authority zinasema kuwa, simu hiyo imeonekana kwenye tovuti ya tume ya mawasiliano ya nchini China kwaajili ya kupewa kibali.
Simu hiyo imeonekana kwenye tovtui hiyo ikiwa imepewa jina la “NEO-AL00” ambapo simu hiyo imeandikwa kuwa na uwezo wa ukubwa wa ndani wa GB 512 pamoja na RAM ya GB 6. Hata hivyo TENAA ni tovuti ya mawasiliano ya nchini china, ambapo simu zote nchini humo huwekwa hapo ili kupewa vibali hivyo huwenda simu hii ikafika kwa watumiaji au isifike kutokana na matokeo ya kupewa kibali hicho.
Kwa sasa bado hakuna simu yenye uwezo huo wa GB 512, Lakini kampuni ya Samsung hapo December mwaka jana ilitangaza kupitia tovuti yake ya habari kuwa, inajiandaa kutengeneza aina mpya ya vifaa vya ukubwa wa ndani (UFS) kwaajili ya simu janja, ambapo vifaa hivyo vitakuwa na uwezo wa kuweka ukubwa wa ndani kwenye simu janja wa GB 512.
Huawei inajiandaa kuzindua simu zake mpya za Huawei P20, simu inayotarajiwa kuja na kamera tatu kwa nyuma pamoja na muonekano na uwezo mzuri zaidi ya simu ya Huawei P10 simu ya jana mwaka jana kutoka mfululizo wa simu za Huawei P.
Samahani kama nitakuwa nimetoa nje ya mada
Msaada Jinsi ya kudownload na kupata orodha yote ya nyimbo za msanii
jinsi ya kupata nyimbo nifuate inbox nitakujuza zaidi