Mtaalamu wa Teknolojia Stephen Hawking Afariki Dunia Leo

Dunia imepoteza mwana sayansi na mwana teknolojia bora.
 Stephen Hawking  Stephen Hawking

Habari za kusikitisha kutoka huko Uingereza, Daktari wa fizikia wa Uingereza ambae pia ni mtaalamu wa maswala ya anga pamoja na teknolojia Stephen Hawking amefariki dunia leo tarehe 14 march 2018 akiwa na umri wa miaka 76. Taarifa za kufariki kwa mwana teknolojia huyo zimesamba leo kupitia mitandao mbalimbali huku zikisikitisha sana watu wengi hasa wafuatiliaji wa teknolojia mbalimbali za anga.

Stephen Hawking amekua mstari wa mbele kufanya tafiti mbalimbali za anga huku akiwa maarufu zaidi kwa nadharia zake kuhusu kuwepo kwa viumbe wengine kwenye anga maarufu kama Alien. Stephen Hawking pia amekua ni muandishi wa vitabu mbalimbali vya maswala ya sayansi ya anga kama vile kitambu cha A Brief History of Time, kilicho mpa umaarufu mkubwa.

Advertisement

Siku za karibuni Stephen Hawking alikuwa mstari wa mbele kuzungumza juu ya kupinga kwa ujio wa mfumo wa Ubunifu wa akili maarufu kama Artificial Intelligence, Huku akisistiza mfumo huo sio mzuri kwa maisha ya badaae ya binadamu.

Akiwa na miaka 21 Stephen Hawking, aliagundulika na ugonjwa wa ALS au (Amyotrophic Lateral Sclerosis) ugonjwa ambao hasa unahusisha seli za neva (neurons) zinazohusika na misuli kufanya kazi kwa hiari. Hata hivyo baada ya kujulikana na ugonjwa huo, Hawking alipewa miaka miwili ya kuishi na madaktari kitendo ambacho alikikataa japokuwa ugonjwa huo uliendela kufanya viungo vya mwili wake kutokufanya kazi zaidi kadri siku zilipo kwenda. Hawking ameacha watoto watatu ambao ni Robert Hawking, Lucy Hawking pamoja na Timothy Hawking.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use