Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video : Mark Zuckerberg Aelezea Sakata la Cambrige Analytica

Hatimaye baada ya ukimya Mark Zuckerberg aomba radhi kwa watumiaji wa FB
facebook Cambrige Analytica facebook Cambrige Analytica

Sakata la Cambrige Analytica bado linaendelea na siku ya jana mgunduzi na mwenyekiti mtendaji wa mtandao wa Facebook alitangazia umma ya watumiaji wa mtandao huo ikiwa pamoja na kuwaomba dhari watumiaji wa mtandao huo kwa ujumla, kwani anajua wamepoteza uaminifu na mtandao huo.

Advertisement

Kwa wale ambao hawajui kuhusu sakata hili ni kuwa, Inasemekana kuwa kampuni ya Cambridge Analytica ilikuwa inatumia data za watumiaji wa mtandao wa Facebook zaidi ya Milioni 50.

Kwa mujibu wa Christopher Wylie, ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya Cambridge Analytica na ambaye ndio aliyefichua sakata hili zima alisema kuwa, data hizo zilikuwa zikitumika kwa wananchi wa marekani kupitia mtandao wa Facebook ambapo matangazo ya uchaguzi wa raisi Donald Trumb yalikuwa yakitumwa kwa wananchi hao ili kufanya ushawishi wa kumchagua raisi hiyo.

Kwenye maojiano na mwandishi wa CCN, Mark amesema kuwa facebook inafanya juhudi za ziada kuhakikisha watumiaji wake wanaamini tena mtandao huo na kwa kuanza facebook itatengeneza sehemu mpya ambapo watu wote walio adhiriwa na uvujaji wa data hizo wataweza kujua na kujifunza njia zaidi za kujilinda.

Siku chache zilizopita hisa za kampuni ya Facebook zimeendelea kushukua kutokana na sakata hilo huku idadi ya watumiaji wa sehemu ya matangazo kupitia mtandao huo pia ikionekana kushuku kwa kasi na kusababisha hisa za kampuni hiyo kushuka kwa zaidi ya asilimia 2.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use