Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps# 4 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Jaribu Programu hizi kwenye simu yako ya Android sasa
App Bora App Bora

Soko la Play Store limejaa App mbalimbali ambazo wengi wetu hatuzi, ndio maana Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha tunakuletea App bora za kujaribu kwenye simu yako ya Android, app hizi bora zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii ya leo.

1. AirConsole – Multiplayer Game Console

App hii itakusaidia kuweza kucheza game kwenye simu yako kupitia kompyuta, yaani kwa kutumia app hii unaweza kubadilisha simu yako kuwa kichezeo Game (Controller) kwenye kompyuta yako au hata wale wenye kutumia TV zenye mfumo wa Android.

Advertisement

2. AmpMe – Play Music Louder on YouTube & Spotify

AmpMe ni App ambayo itakusaidia kucheza nyimbo au muziki fulani kupitia vifaa vyako vyote vya Android. Yaani kwa kutumia app hii utaweza kucheza muziki fulani kwenye simu yako na utaweza kuwezesha muziki huo huo kucheza (kuimba) kwenye simu nyingine kwa wakati mmoja, app hii inafanyakazi hata kwa mitandao kama youtube na Spotify.

3. Snapseed

Snapseed
Price: Free

Snapseed ni programu kutoka Google, programu hii inakupa uwezo wa hali ya juu sana wa kuweza ku-edit picha kwenye simu yako ya mkononi. Snapseed inakupa uwezo wa kuchagua filter mbalimbali pamoja na uwezo mkubwa wa kufanya picha yako kuonekana vizuri zaidi.

4. Assistive Touch

Assistive Touch ni programu ya android itakayo kusaidia kuweza kuweka kitufe ambacho kitakusaidia kutumia simu yako kwa urahisi. Kitufe hichi kitaweza kuwekewa programu mbalimbali ambazo utaweza kuzitumia kwa haraka kwa kubofya kitufe hicho.

5. Computer Launcher

App ya mwisho kwenye list hii ni Computer Launcher, App hii itakusaidia kuweka muonekano wa kompyuta ya windows kwenye simu yako. Kama wewe ungependa kupata muonekano wa kompyuta kwenye simu yako basi jaribu app hii kwenye simu yako ya Android.

Na hizo ndio programu au App ambazo nimekuandalia siku ya leo kama ulipitwa na list iliyopita unaweza kusoma hapa list ya App nyingine za kujaribu kwenye simu yako ya Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use