Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Yazindua iPad (2018) ya Inch 9.7 Kwaajili ya Wanafunzi

Soma hapa sifa za iPad (2018) pamoja na Bei yake kwa hapa Tanzania
iPad (2018) iPad (2018)

Kabla hujalala ningependa nikupe taarifa moja ya muhimu kuhusu kampuni ya Apple, Kwani hivi leo kampuni hiyo imezindua iPad (2018) mpya kwaajili ya wanafunzi, iPad hiyo yenye inchi 9.7 inakuja na kalamu maalum ambayo itasaidia kufanya mambo mbalimbali kwa wanafunzi.

Advertisement

iPad hii haina tofauti sana na iPad ya mwaka jana bali kikubwa ambacho ni tofauti ni kuwa iPad hii sasa inauwezo wa kutumia kalamu maalum ambayo hapo hawali ilikuwa inafanya kazi kwenye iPad Pro. iPad (2018) inakuja na Touch ID, HD FaceTime kamera, battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 10, kamera ya nyuma ya megapixel 8, mfumo wa mtandao wa 4G LTE huku vyote vikiwa vinaendeshwa kwa processor ya Apple’s A10 Fusion chip.

Sifa za iPad (2018) inch 9.7

  • Uzito –  469g (1.03 pounds)
  • Vipimo: 240 x 169.5 x 7.5mm
  • Ukubwa wa Kioo: 9.7-inch
  • Resolution: 2048 x 1536
  • Uwezo wa Processor: A10 Fusion Chip
  • Mfumo wa Uendeshaji: iOS 11
  • Ukubwa wa Ndani: 32GB/128GB
  • Kamera ya Nyuma: 8MP
  • Kamera ya Mbele: 1.2MP Facetime HD
  • Uwezo wa Battery: up to 10 hours
    Touch ID, Pencil Support, up to 300Mbps LTE

iPad (2018) inategemewa kuingia sokoni kuazia kwa siku ya leo kwa dollar za marekani $299 kwa shule na kwa watumiaji wa kawaida $329, hii ikiwa ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 677,000 kwa shule na Tsh 744,400 kwa watumiaji wa kawaida. Vilevile kalamu maalumu ya Apple itauzwa kwa dollar za marekani $89 kwa wanafunzi na dollar $99 kwa watumiaji wa kawaida. Hii pia ikiwa ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 201,400 kwa shule na Tsh 225,000 kwa watumiaji wa kawaida.

Maalum kwa wanafunzi Apple wameongeza ukubwa wa iCloud kutoka GB 5 hadi GB 200 na hii itakuwa maalum kwaajili ya wanafunzi pekee. Makadirio ya Bei hizo hapo juu ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, kumbuka bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania ukichangaya na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use