Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 11/3/2018

Hizi ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki Hii
Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 11/3/2018 Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 11/3/2018

Karibuni tena wana teknolojia ni wiki nyingine tunakutana kwenye makala za Tech Wiki, leo ikiwa ni siku ya jumapili ya tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka 2018, tunaenda kuangalia habari zote za teknolojia zilizoshika chati hapa Tanzania Tech. Basi bila kupoteza muda twende nikujuze..

Wiki hii kampuni ya Samsung ilifanya mapinduzi ya teknolojia kwa kutambulkisha sokoni TV zake mpya za QLED 2018 zenye uwezo wa kufanana na Ukuta. TV hizo zinatumia teknolojia mpya ya Ambient Mode ambayo inaruhu TV yako kuweza kufanana na ukuta wa mahali ulipo iweka.

Advertisement

Hivi karibuni ripoti kutoka kwa wachambuzi makini wa teknolojia zinasema, Apple inatarajia kuja na Laptop mpya mwaka huu na moja ya laptop hiyo ni MacBook Air ambayo itakuwa ikiuzwa kwa bei rahisi zaidi.

Bado teknolojia inaendelea kushika chati hadi kwenye jiko lako, kudhibitisha hilo hivi karibuni huko inchini marekani kumegunduliwa roboti anae itwa Flippy yenye uwezo wa kupika Burger zaidi ya 150 kwa lisaa limoja tu.

Habari nyingine kubwa ya teknolojia wiki hii inatokea Tanzania, Ripoti kutoka kwenye gazeti la habari leo zinasema kuwa hivi karibuni zanzibar itanza kutengeneza simu kutokana na kuingia mkataba na kampuni ya korea, Utengenezaji wa simu hizo utanza kwa awamu na utanza kwa ku-unganisha vifaa vya simu na baadae mwaka 2020 kutengeneza simu kabisa.

Habari nyingine kubwa ya teknolojia wiki hii ni kuhusu simu mpya ya huawei, simu hii inasemekana kuja na kamera tatu kwa nyuma pamoja na maboresho zaidi. Simu hii inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 27 mwezi huu wa tatu 2018.

Tumesha zoea instagram ndio huiba vitu kutoka kwa snapchat, lakini sasa snapchat ndio inachukua sehemu ya mention kutoka Instagram. Sehemu hii inafanana na sehemu ya kwenye instagram ambapo utaweza kumtag mtu kwenye picha au video zako za Stories kupitia Snapchat.

Habari nyingine kubwa na njema kwa Tanzania wiki hii ni pamoja na Google kuruhusu watengenezaji wa programu za Android kuanza kuuza App zao kupitia soko la Play Store. Tanzania ni nchi pekee afrika mashariki iliyo ruhusiwa kuweza kuuza App kupitia Soko hilo.

TTCL kwa mwaka huu imekuja kwa vigingine ikiwa pamoja na kuwataka wananchi kuweza kupata laini za mtandao huo bure kwa kutangaza kuwa laini za mtandao huo zinatolewa bure kabisa na Haziuzwi na endapo mtu akiuziwa laini hizo ni vyema kutoa taarifa kwa kampuni hiyo.

Habari ya mwisho ya teknolojia kwa wiki hii ni kuwa, Instagram inakuja na sehemu mpya ya Portrait Mode ambayo inaitwa “Focus”. Sehemu hii inapatikana kwenye kamera za simu nyingi za siku hizi, sehemu hii inakusaidia kuweza kuchukua picha ya eneo la mbele la kitu unachotaka kupiga picha huku kwa nyuma kukiwa hakuonekani vizuri. Yaani kama sehemu ya Auto Focus inavyofanya kazi.

Na hizo ndio habari za teknolojia kwa wiki hii ya jumapili ya tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka 2018. Kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita unaweza kusoma hapa habari zote kubwa kwa wiki hiyo. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use