Hivi karibuni Google imenza kufanya maboresho kwenye soko lake la Play Store, huku moja ya maboresho hayo yakiwa ni pamoja na kuruhusu nchi ya Tanzania kuweza kuuza App kwenye soko hilo la programu za Android.
Kipindi cha nyuma wabunifu wa programu za Android walikuwa hawawezi kuuza programu kwenye soko hilo kitendo ambacho kilikuwa kina walazimisha wabunifu wengi kutengeneza App za bure zenye matangazo mengi ili kuweza kukidhi kipato kinacho tokana na kazi ya utengenezaji wa programu hizo.
Taarifa hizo zimeandikwa leo kupitia tovuti ya Google ambapo nchi ya Tanzania imeorodhesha kwenye list ya moja ya nchi ambazo zitakuwa na uwezo wa kuuza App kwenye soko lake la Play Store ikiwa pamoja na uwezo wa kusajili akaunti ya mauzo. Kwa sasa watengenezaji wa programu wataweza kuuza programu zao moja kwa moja kupitia soko hilo.
Kama tayari unayo akaunti ya kuweka App kwenye soko la Play Store, ingia kwenye uwanja huo kisha bofya kwenye sehemu ya Payment Settings na hapo utaweza kujaza fomu maalum ya kujiunga na huduma ya kuuza programu kupitia soko hilo. Tanzania ni nchi pekee kwa Afrika mashariki iliyo ruhusiwa kuuza App kupitia soko hilo, pengine hizi ni juhudi za wana teknolojia mpaka Google imeweza kuona umuhimu wa kuleta huduma hiyo hapa nchini.
Pengine pia hii ni hatua nzuri ya Google kwenda kuruhusu matangazo yake kwenye tovuti mbalimbali za kiswahili. Endelea kutembelea Tanzania Tech bila shaka tutakuwa hapa kuweza kukujuza pindi siku hiyo itakapo fika.
Asante sana Double T kwakutupatia habari kila wakati
Karibu sana
Awesome