Hivi karibuni, Kampuni ya samsung ilivunja rekodi kwa upande wa teknolojia kwa kuja na Hard Disk kubwa ya SSD yenye ukubwa wa Terabyte (TB) 30. Lakini muda umepita na tayari kampuni ya Samsung imesha pokonywa taji hilo na kwa sasa taji la Hard Disk kubwa kuliko zote duniani, linaenda kwa kampuni ya Nimbus ambayo imetengeneza Hard Disk ya SSD yenye ukubwa wa Terabyte (TB) 100.
Hard Disk hiyo ya ExaDrive DC100 kwa sasa inafanyiwa majaribio kwa wateja wachache huko nchini marekani, huku kampuni ya Nimbus ikiahidi kuleta Hard Disk hiyo kwa wateja wote siku za karibuni.
Kwa upande wa uwezo, Hard Disk hii ya TB 100 inakupa uwezo wa kutuma na kupokea vitu kwa kasi ya MB 500 kwa sekunde huku ikiwa na uwezo wa kuhifadhi Filamu za HD zenye ukubwa wa GB 2 zaidi ya filamu 20,000, Kama wewe ni mpenzi wa muziki kupitia Hard Disk hii unaweza kuhifadhi zaidi ya nyimbo milioni 20.
Hata hivyo bado haijajulikana bei ya Hard Disk hii, lakini ni vyema kutegemea kuwa haitakuwa bei rahisi kwani kwa mujibu wa tovuti ya Theverge, kampuni ya Nimbus haija tengeneza Hard Disk hiyo maalum kwa mtumiaji mmoja lakini zaidi kwa ajili ya makampuni.
Itakapotajwa bei tujulishe basi