Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii Tarehe 25/03/2018

Hizi hapa ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii
Habari za Teknolojia Wiki Hii Habari za Teknolojia Wiki Hii

Habari mwana teknolojia ni siku nyingine tena tunakutana kwenye mkusanyiko wa habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii ya tarehe 25/03/2018. Kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki hii, soma hapa kuweza kujua yote yaliojiri na kuhabarika kwa urahisi zaidi.

Wiki hii sakata jipya limeibuka na kuchukua sura mpya ambapo facebook inalaumiwa kuruhusu kampuni ya Cambrige Analytica kuchukua data za watumiaji wa mtandao huo kinyume na sheria ili kumsaidia raisi Donald Trump kuweza kushinda uchaguzi wa uraisi hapo mwaka 2016. Sakata hili limechukua vichwa vya habari kwenye tovuti nyingi za habari za teknolojia huku mwenyekiti mtendaji wa mtandao wa facebook, Mark Zuckerberg akiwaomba radhi watumiaji wa mtandao huo kutokana na sakata hilo.

Advertisement

Habari nyingine kubwa ya teknolojia kwa wiki hii ilikua inatokea Tanzania, Ambapo inasemekana kuna wizi mpya wa fedha benk ambapo wezi huweza kutumia wi-fi bandia kuweza kuchukua nyaraka zako za siri za bank kama vile PIN, Password au Nywila na taarifa nyingine za siri.

Habari nyingine kubwa ya teknolojia wiki hii ilikuwa inatokea marekani kwenye kampuni ya Apple, ambapo kampuni ya Apple inajiandaa kufanya mkutano mkubwa wa elimu ambao utafanyika huko chicago nchini marekani siku ya jumanne ya tarehe 27 mwezi huu wa tatu. Kwenye Mkutano huo unatarajiwa kuwa na uzinduzi wa bidhaa za Apple kwaajili ya Wanafunzi.

Wiki hii kampuni ya IBM kupitia mkutano wake wa IBM Think 2018, ilizindua kompyuta ambayo inasemekana ndio ndogo kuliko zote duniani, Kompyuta hii ni ndogo kuliko hata chembe ya chumvi na ina uwezo wa kufanya kazi mbalimbali kama vile kugundua wizi, kugundua njia za usafirishaji pamoja na kufanya kazi za mfumo wa AI.

Baada ya kutoka kwenye kompyuta ndogo kuliko zote wiki hii pia ilizinduliwa Hard Disk kubwa kuliko zote duniani. Hard Disk hii ya mfumo wa SSD ina Terabyte 100 sawa na GB 100,000. Hard Disk hii  imezinduliwa siku ya jumatatu ya tarehe 18 na kampuni ya Nimbus ya nchini Marekani.

Wiki hii pia, Google ilikuwa kwenye habari kubwa za teknolojia kwa kuzindua njia mpya ambayo utaweza kujaribu Game kupitia Play Store bila kupakua au ku-nstall game hiyo kwenye simu yako. Unachotakiwa ni kutafuta game hizo, kisha bofya TRY NOW na utaweza kujaribu game hiyo bila kupakua kwenye simu yako.

Kwa wale ambao ni wapenzi wa game, habari hii ilikuwa kubwa sana kwao kwani game ya PUBG au PlayerUnknown’s Battlegrounds ni moja ya Game pendwa sana kwenye mifumo mbalimbali ya Xbox, PS4 na mifumo mingine. Game hii siku za karibuni imepata umaarufu mkubwa mpaka kushirikisha wasanii wakubwa kama Drake wakionyesha ujuzi wao katika kucheza game hii kupitia mtandao wa Twitch.

Kampuni ya kutengeneza simu ya HTC nayo ilikuwa kwenye habari kubwa za teknolojia wiki hii huku ikiwa na simu mpya ya HTC Desire 12 pamoja na HTC Desire 12 Plus ambazo zinakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32, Kamera mbili kwa nyuma zenye Megapixel 12 na Megapixel 2 simu hizi zinategemewa kuingia sokoni siku za karibuni.

Habari nyingine za kusikitisha wiki hii, Msichana mmoja nchini india amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na simu ya Nokia aliyokuwa akiongelea huku akiwa ameweka simu hiyo kwenye chaji. Inasemekana kuwa simu hiyo baada ya kulipuka ilimjeruhi sehemu ya kifua na mkono majeraha ambayo yalimsababishia umauti akiwa hospital.

Tukitoka kwenye masikitiko hayo, Turudi kwenye simu mpya kwa mwaka huu 2018 ambapo, kampuni ya Lenovo imeingiza sokoni simu zake mpya tatu zenye kuvutia ambazo ni Lenovo S5, Levone K5 pamoja na Lenovo K5 Play. Simu kiukweli ni nzuri sana kwa sura huku zikiwa na rangi nzuri za kuvutia.

Mwanzoni wote tunajua kuwa ilikuwa inakubidi uwe na programu maalum ndipo uweze kuchukua video za mubashara kupitia kamera ya kompyuta yako. Lakini wiki hii youtube imeleta njia mpya kabisa ya kurahisisha kurekoni video za mubashara ambapo sasa unahitaji kuwa na kisakuzi cha Google Chrome tu, na hapo utakuwa uko tayari kurekodi video za mubashara kwa kutumia kamera ya kompyuta yako au (Web Cam).

Habari nyingine ya teknolojia ambayo pia ni ripoti kwa wiki hii, Inasema kuwa kampuni ya Huawei inategemewa kuja na simu yake mpya ambayo inasemekana kuja na ukubwa wa ndani wa Hadi GB 512. Ripoti hii inatokana na jina na sifa za simu hiyo kuonekana kwenye tovuti ya mawasiliano ya china kwaajili ya kupewa kibali.

Wiki hii pia instagram haikuwa nyuma, Kwani ilikuja na habari ya kuwa sasa utaweza kuweka hashtag pamoja na kumtag mtu kupitia kwenye sehemu ya Bio ndani ya ukurasa wa Instagram. Sehemu hiyo kwa sasa nafanya kazi unaweza kujaribu kufanya hivyo sasa.

Wiki hii pia kulikuwa na habari za iPhone, ambapo kampuni moja ya nchini urusi ambayo inajihususha na utengenezaji wa vifaa vya thamani, ilikuja na simu ya iPhone X iliyotengenezwa kwa dhahabu. Simu hii ina sura ya raisi uwa urusi kwa nyuma ikiwa kama ishara ya kumpongeza raisi huyo kwaajili ya kushinda uchaguzi wa raisi nchini humo.

Habari nyingine kubwa ya Teknolojia zilikuwa zinatokea Tanzania ambapo wiki hii, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), imewaagiza wafanya biashara waliosajili kampuni kabla ya February mosi, 2018 kuhakiki taarifa ili ziingizwe katika mfumo mpya wa kusajiliwa biashara kwa njia ya mtandao.

Wiki hii habari nyingine kubwa ya teknolojia inamuhusu Elon Musk, ambapo wiki hii mkurugenzi wa makampuni hayo ya Tesla na SpaceX alifuta kurasa za facebook za kampuni zake hizo kutokana na mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter kumshinikiza Afanye hivyo. Hata hivyo hii inatoka na sakata la Facebook linalo endelea hadi sasa.

Habari nyingine kubwa kwa wapenzi wa kupakua video ni kuwa, Tovuti maarufu ya Keepvid hivi karibuni imesimamisha huduma zake na sasa hutoweza kupakua video bali sasa utapa ushauri wa kuzingatia wakati wa kupakua video ikiwa pamoja na takwimu za upakuaji wa video.

Wiki Hii kampuni ya Samsung nchini india, imeingiza ingizo jipya la simu ya J7 Prime ambapo sasa utaweza kupata simu ya J7 Prime 2 ambayo itakuwa imeboreshwa zaidi pamoja na kuongezewa kamera kubwa za Megapixel 13 kwa mbele na nyuma.

Habari njema kwa wapenzi wa simu za tecno wiki hii, tetesi zimeibuka kuwa tecno inatarajia kuzindua simu yake mpya ya Tecno Camon X ambayo itakuwa na uwezo mkubwa wa Kamera ambayo inatarajiwa kuja na ukubwa wa Megapixel 60. Simu hii pia inasemekana kuja na teknolojia mpya ya kupo-oza simu ili kufanya ifanye kazi vizuri, Tecno Camon X inatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao nchini Nigeria lakini tarehe bado haijajulikana.

Na hizo ndio habari za teknolojia kwa wiki hii ya tarehe 25/03/2018, Kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita unaweza kusoma habari hizo kupitia hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use