Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii 18/3/2018

Hizi hapa habari zote kubwa za teknolojia kwa wiki Hii
Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii 18/3/2018 Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii 18/3/2018

Kama ulipitwa na Habari za Teknolojia kwa wiki hii, Makala hii itakuletea mkusanyiko wa habari kubwa za teknolojia za wiki nzima ili kurahisisha kujua yote yale yalio jiri kwenye ulimwengu wa teknolojia kwa wiki hii ya tarehe 18/3/2018.

Kwa wale ambao hamfahamu kuhusu Stephen Hawking, Huyu ni mwana fizikia ambaye anajulikana sana kwa utaalamu wake wa masuala ya Anga. Stephen Hawking alifariki siku ya Jumatano Asubuhi akiwa na umri wa miaka 76 japokuwa madaktari wake walimwambia angefariki miaka miwili baadae baada ya kupata ugonjwa wa ALS.

Advertisement

Kampuni ya simu ya Huawei Wiki hii ilizindua simu mpya ya Huawei Y9 simu ambayo inakuja na sifa za RAM GB 3, Ukubwa wa ndani GB 32, Kamera za mbele ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine Megapixel 2 na Kamera za nyuma pia ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine megapixel 2, Simu hii inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8.0 Oreo na itauzwa kwa bei ya Tsh 600,000 bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania.

Hatimaye wiki hii mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Airtel Tanzania yameanza rasmi ili kuweza kutatua mgogoro wa nani ni mmiliki halali wa kampuni hiyo ya simu ambayo kwa sasa asilimia kubwa za hisa zinamilikiwa na kampuni ya Bharti Airtel.

Kama umekua ukifuatilia Tanzania Tech utajua kuhusu sehemu ya Delete For Everyone, sehemu hii inakuruhusu kufuta meseji uliyo tuma kwa kosea na itafutika kwa mtu uliye mtumia. Sasa hapo hawali sehemu hii ilikuwa inakuwezesha kufuta meseji ambazo umekosea ndani ya dakika 7, lakini sasa unaweza kufuta meseji ulizo kosea hadi za lisaa limoja lilopita.

Mtandao wa YouTube wiki hii umefanya mabadiliko kwa kuleta sehemu mpya ya Dark Theme kwenye App zake za Android pamoja na iOS. Sehemu hii itakusaidia kuweka weusi kwenye App za Youtube ili kuweza kuzuia matatizo ya macho hasa wakat wa usiku.

WhatsApp wiki hii imeleta uwezo wa kuweka maelezo ya Group yaani Group Description, sehemu hii itakusaidia wewe Admin kuweza kueleza Group lako lina husu nini au unaweza kuandika sheria za Group na mtu ataweza kuziona kabla na mara baada ya kujiunga na Group hilo.

Wiki hii kampuni ya Spotify imeingia Afrika kwa mara ya kwanza na kufungua tawi la kampuni hiyo nchini Afrika ya Kusini. Msemaji wa Spotify pia amesema Afrika Kusini ni hatua ya kwanza hivyo pengine tutegemee mtandao huo kuja Tanzania kwa siku za Kariibuni.

Mwalimu wa kompyuta nchini ghana ambaye alikuwa gumzo mwezi uliopita kwa kuchora kompyuta ubaoni kwaajili ya kufundisha wanafunzi. Wiki hii ameposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii akionyesha misaada aliyopokea baada ya picha hiyo kufikia kampuni ya kompyuta ya Microsoft Afrika. Mwalimu huyo pia ameonyesha jinsi alivyo kwenda huko Singapore kwaajili ya mafunzo zaidi ya kompyuta.

Wiki hii wataalamu kutoka kampuni ya Toyota walionyesha roboti yenye uwezo wa kutupa mipira ya Kikapu bila kukosea hata kidogo. Roboti hiyo inayo itwa Cue ilishindanishwa na binadamu na kuweza kushinda kwa asilimia 100, Roboti hiyo inatumia mfumo wa AI kuweza kutupa mipira hiyo bila kukosea.

Habari yamwisho kubwa kwa upande wa Teknolojia kwa wiki inamuhusu mwanamuziki rihanna, Wiki hii mwanamuziki huyo alitoa maneno makali kwa mtandao wa Snapchat baada ya kuruhusu tangazo lisilokuwa na maadili ambalo lilikuwa likitaka watu kuchagua wa kumpiga kati ya Rihanna na mpenzi wake wa zamani Chris Brown. Tangazo hilo lilikuwa ni la mchezo maarufu wa Would You Rather ambapo unatakiwa kuchagua chaguo moja gumu kati ya machaguo mawili yaliyo wekwa.

Na hizo ndo habari za Teknolojia kwa wiki hii kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita ya tarehe 11/3/2018 unaweza kusoma habari hizo kupitia hapa. Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pamoja na App Store.

1 comments
  1. hivi kiongozi samahani nataka kujua nawezaje kuweka maneno kwenye video nitakazo rusha YouTube kama Yale mf.”Kupata hari zaidi usisahau Ku subscriber”
    pia kuweka logo yangu kwenye video husika niliyotuma mf. wako ukituma iwe Tt au kama ITV na n.k

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use