Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Imetangaza Kuzima Tovuti Yake ya Link ya Goo.Gl

Link zitaendelea kufanya kazi lakini hutoweza kutengeneza link mpya
Google URL Shortener Google URL Shortener

Kampuni ya Google inajulikana kwa kuwa na tovuti mbalimbali ambazo zimekua msaada mkubwa miongoni mwa watumiaji wake, Hivi karibuni Google kupitia blog yake imetangaza kuzima tovuti yake ya kufupisha link inayoitwa Google URL Shortener. Tovuti hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kuweza kubadilisha link ndefu kuwa fupi ili kurahisisha pale unapotaka kushiriki link hizo na watu wengine.

Google kupitia ukurasa wake huo imeandika kuwa, kuanzia tarehe 30 mwezi huu google haitakuwa inaboresha tena tovuti ya Google URL Shortener na pia kuanzia tarehe 13 ya mwezi wa nne watu ambao tayari walishakuwa wanatumia tovuti hiyo ndio watakao weza kuendelea kutumia tovuti hiyo. Kwa wale ambao hadi kufika tarehe 13 Aprili 2018 watakuwa bado hawaja anza kutumia tovuti hiyo basi hawato weza kutumia tovuti hiyo kabisa.

Advertisement

Google pia imeandika kuwa, kwa wale ambao watawezeshwa kuendelea kutumia tovuti ya Google URL Shortener wataendelea kutumia huduma hiyo hadi kufikia mwakani 2019 ambapo huduma hiyo itasitishwa kabisa. Google imeongeza kuwa link zote zitaendelea kufanya kazi kama kawaida ila watumiaji hawatokuwa na uwezo wa kutengeneza link mpya ikiwa pamoja na kupata data za link hizo.

Kwa sasa Google imesema inawashauri watu wanao hitaji kuendelea kufupisha link, kutumia huduma nyingine za kufupisha link kama vile huduma za Bitly pamoja na Ow.ly, Kwa ripoti kamili kuhusu hili unaweza kusoma habari hiyo hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use