Teknolojia bado inaendelea kushika chati kila upande, kudhibitisha hayo hivi karibuni wataalamu kutoka Miso Robotics wamegundua roboti yenye uwezo wa kutengeneza burger inayoitwa “Flippy”.
Roboti hiyo ambayo sasa inafanya kazi ya kutengeneza Burger kwenye mgahawa wa Cali Burger uliopo huko Southern California, inakadiriwa kuwa na uwezo wa kutengeneza Burger mpaka 150 kwa lisaa limoja. Kwa kutumia mkono wake unao julikana kitaalam kama six-axis robotic arm, Flippy inauwezo wa kutengeneza Burger kwa kupokea oder kupitia mfumo maalum wa tiketi za kidigital.
Roboti hiyo ya Flippy inatumia mifumo mingine mbalimbali ili kuweza kukamilisha kazi ya kupika burger, mifumo hiyo ni pamoja na mifumo ya kutupima joto, mifumo ya picha pamoja na mifumo ya kutumia kamera na hii ni kusaidia kuangalia kiwango cha upikaji kwenye kila burger inayopikwa. Mbali na hayo Flippy pia inaogozwa na binadamu kwa kufanya uangalizi wa muda ikiwa pamoja na kuhakiki kuiva kwa Burger kwa kutumia kamera.
Kwa sasa roboti hiyo ya Flippy bado iko kwenye hatua za majaribio ya miezi sita kwenye mgahawa huo na endapo majaribio hayo yakifanikiwa basi roboti hiyo inategemewa kuingia sokoni kwa dollar za marekani $60,000 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 135,264,000 na hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.
Je vipi unaonaje Roboti hii, unadhani roboti hii itakuwa na uwezo wa kutengeneza Burger vizuri kama binadamu wanavyo tengeneza..? na vipi kuhusu ajira..? je roboti hii inatafaa kwa hapa Tanzania ukizingatia tunaelekea kwenye Tanzania ya viwanda..? tuambie maoni yako hapo chini.