Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Ndani ya Kashfa Nzito ya Kuvujisha Data za Faragha

Facebook inadai hakuna uvujishaji wa data zozote uliofanyika
Facebook Ndani ya Kashfa Nzito ya Kuvujisha Data za Faragha Facebook Ndani ya Kashfa Nzito ya Kuvujisha Data za Faragha

Wiki hii kashfa nzito imeibuka baada ya mtandao maarufu wa Facebook kuhusishwa na uvujishaji wa data za siri za watumiaji wake kupitia kampuni ya uchambuzi ya Cambridge Analytica ambayo ilikuwa inamuunga mkono raisi Donald Trump katika kampeni yake ya uraisi mwaka 2016.

Inasemekana kuwa kampuni ya Cambridge Analytica ilikuwa inatumia data za watumiaji wa mtandao wa Facebook zaidi ya Milioni 50 kitendo ambacho kilipingwa na kufanya Facebook kuifungia kampuni hiyo kutumia mtandao wa Facebook kwa ujumla.

Advertisement

Aidha haijaishia hapo sakata zima limeanzia baada ya profesa mmoja wa Cambridge kutengeneza App yake ya “thisisyourdigitallife” ambayo ilikuwa inawezesha watumiaji kuingia kwenye App hiyo kwa kutumia mfumo wa kuingia wa Facebook Login.

Hata hivyo App hiyo ili pakuliwa na watu zaidi ya 270,000 na baadae inasemakana profesa huyo aliuza data za watumiaji wa App hiyo kwa kampuni ya Cambridge Analytica ambapo inasemekana kampuni hiyo ilitumia data hizo kumsaidia ushindi raisi Donald Trump.

Kampuni ya Cambridge Analytica inasemekana kuweza kuchukua data za watumiaji zaidi ya walio pakua app kwa kutumia njia ya kuchukua data za watu wa karibu wa watumiaji wa App hiyo ambao tayari walisha ipakua App hiyo.

Hata hivyo japokuwa inasemekana yote haya yalikuwa yanawezeshwa na aina ya mpangilio au settings ambazo watumiaji hao walikuwa wamechagua ndani ya profile ya mtumiaji wa App hiyo lakini bado inatajwa kuwa hii ilikuwa ni kinyume na sheria za mtandao wa facebook.

Kwa mujibu wa Christopher Wylie, ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya Cambridge Analytica na ambaye ndio aliyefichua sakata hili zima alisema kuwa, data hizo zilikuwa zikitumika kwa wananchi wa marekani kupitia mtandao wa Facebook ambapo matangazo ya uchaguzi wa raisi Donald Trumb yalikuwa yakitumwa kwa wananchi hao ili kumewezesha raisi huyo kushinda kwenye uchaguzi wa uraisi hapo mwaka 2016.

Kwa mujibu wa mtandao wa Quartz, Baada ya Facebook kugundua kuwa app hiyo inatumia data za watumiaji wake kinyume na sheria. Facebook ilichukua hatua ya kuzuia na kufuta App hiyo kwenye mtandao wa Facebook na kuhitaji uhakikisho kuwa data zote zilizopatikana kutoka kwa watumiaji wake zilifutwa na hazikutumiwa kwa namna yoyote, Hata hivyo inasemekana Facebook haikufuatilia zaidi kuhakikisha kama data hizo zimetumiwa ama lah!.

Mpaka sasa bado kampuni ya Facebook inakataa tuhuma hizi huku kisema kuwa hakuna uvujishaji au uchukuaji wa data za zaidi uliofanyika na kampuni hiyo ya Cambridge Analytica, huku ikisema kuwa data zilizochukuliwa ni zile ambazo watumiaji wa App ya “thisisyourdigitallife” waliruhusu pale walipo pakua App hiyo.

Mpaka sasa bado sakata hili linazidi kuendelea na Facebook imetangaza kufanya mkutano wa wafanyakazi wake hapo kesho na kuruhusu maswali juu ya sakata hilo. Pia inaripotiwa kuwa, idadi ya watu wanaotumia matangazo ya Facebook imepungua  ikiwa pamoja na hisa za mtandao huo baada ya kuibuka kwa sakata hilo tokea siku ya ijumaa ya tarehe 16.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use