Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Brela Yataka Wenye Kampuni Kuhakiki Taarifa Mtandaoni

Muhimu wafanyabiashara waliosajili kampuni kabla ya February mosi, 2018
Brela Yataka Wenye Kampuni Kuhakiki Taarifa Mtandaoni Brela Yataka Wenye Kampuni Kuhakiki Taarifa Mtandaoni

Hivi karibuni, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), imewaagiza wafanya biashara waliosajili kampuni kabla ya February mosi, 2018 kuhakiki taarifa ili ziingizwe katika mfumo mpya wa kusajiliwa biashara kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo hapo Awali, endapo taarifa za wakurugenzi na wanahisa wa kampuni zikiwa halingani na zile za Brela, wenye kampuni walikuwa wanapaswa kusafiri hadi Dar es Salaam kupata baadhi ya huduma ambazo kwa sasa zinapatikana mtandaoni na ndani ya nusu saa badala ya siku saba kama mwanzo.

Advertisement

Ofisa mtendaji mkuu na msajili wa kampuni wa Brela, Frank Kanyusi alisema jana kuwa, uhakiki wa taarifa ni muhimu kwa kuwa unampunguzia mwenye kampuni muda wa kuzunguka. “Uhakiki huo haumlazimu mfanyabiashara kwenda Brela kwani atapaswa kuhakiki hapohapo alipo kwa njia ya mtandao. Maboresho ndani ya taasisi yanamwezesha kila Mtanzania au mfanya biashara kunufaika na huduma zetu,” alisema Kanyusi.

Afisa huyo alisistiza zaidi kuwa, ifikapo mwishoni mwa Aprili, mwaka huu, ofisi yake itazindua mfumo mpya sambamba na utoaji leseni daraja A na B ambapo ile ya daraja A inatolewa na Brela na B itatolewa na ofisi za halmashauri.

“Atapata usajili wa kampuni, TIN na leseni ndani ya saa nne, hivyo leo (jana) kampuni zilizosajiliwa kabla ya Februari mosi 2018 wahakiki taarifa zao kwa kuzingatia mfumo huu mpya ili nazo ziwe katika mfumo, kwa sababu awali uwasilishaji taarifa haukua sahihi,” alisema na kuongeza “Hivyo tunataka wao watuletee taarifa wanazoona ndizo sahihi na tulinganishe na tulizonazo kisha tunakubaliana zipi ni sahihi.”

Alisema taarifa ziingizwe kwenye mtandao badala ya mtu kusafiri hadi Dar es Salaam kuziwasilisha. Mkuu wa kitengo cha kampuni kutoka Brela, Rehema Kitambi alisema wametenga chumba maalumu ofisini kwao kwa ajili ya kuwasikiliza wateja wanaotaka kujisajili kwa njia ya mtandao. “Hivyo (wateja) waje tutawahudumia na kila swali litapata jibu, naamini wakishazoea kila kitu kitakwenda sawa na ufanisi utaongezeka,” alisema.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use