Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Kufanya Mkutano wa Elimu Tarehe 27 March 2018

Apple kuangazia njia za kuboresha elimu kupitia teknolojia tarehe 27
Mkutano wa Apple Mkutano wa Apple

Kampuni ya Apple ambayo inayo makao yake makuu huko Cupertino, California, nchini marekani. Hivi karibuni inategemewa kufanya mkutano wa aina yake ambao utakuwa ukiangazia zaidi kwenye maswala ya elimu.

Kwa mujibu wa tovuti ya theinquire, Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi huu tarehe 27 ambapo, wataalam wa mambo wanasema pengine mkutano huo utatumika kutangaza vifaa vya bei rahisi kutoka kwa kampuni hiyo, kwani mwezi uliopita watafiti wa maswala ya teknolojia walidai kuwa, huwenda kampuni ya Apple ikazindua laptop ya MacBook Air ya bei rahisi tofauti na laptop ya sasa inayozwa bei ghali kuanzia dollar za marekani $999 au zaidi ambayo ni sawa na Tsh 2,260,000 au zaidi kwa ongezeko la kodi kwa Tanzania.

Advertisement

Vilevile habari zinasema kuwa huenda Apple wakazindua iPad mpya ya inch 9.7 kwaajili ya wanafunzi ambayo nayo itakuwa ya bei rahisi kuanzia dollar za marekani $259 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 586,751.55 tofauti na iPad ya sasa ambayo inauzwa kwa dollar za marekani $460 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,042,107.00. Hata hivyo kwa sababu tukio zima litahususha maswala ya elimu, tutegemee kuona baadhi ya programu mpya za Apple kwaajli ya wanafunzi au elimu kwa ujumla.

Tayari kampuni ya Apple imesha anza kutumia mialiko mbalimbali kwaajili ya kuudhuria mkutano huo utakao fanyika kwenye Shule moja ya sekondari huko Chicago nchini marekani.

Kujua zaidi kuhusu mkutano huo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuwa tukikujuza yote yatakayo tokea kwenye mkutano huo mubashara kabisa siku hiyo ya Tarehe 27 march mwaka huu 2018.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use