Afariki Baada ya Kulipukiwa na Simu ya Nokia Nchini India

Simu hiyo ya Nokia ililipuka wakati akiwa naongea huku akichaji
Afariki Baada ya Kulipukiwa na Simu ya Nokia Nchini India Afariki Baada ya Kulipukiwa na Simu ya Nokia Nchini India
<a href="https://www.thesun.co.uk/news/5847110/girl-18-killed-when-nokia-phone-she-was-chatting-on-exploded-after-she-plugged-it-in/" rel="nofollow" target="_blank"><span style="font-size: x-small;">Photo by The Sun</span></a>

Hapo jana ripoti kutoka nchini india zinasema kuwa, Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Uma Oram, mwenye umri wa miaka 18, kutoka Kheriakani nchini India. Amefariki dunia baada ya kulipukiwa na simu ya Nokia 5233 aliyokuwa anatumia.

Aidha ripoti kutoka mtandao wa Metro zinasema kuwa, msichana huyo alikuwa anatumia simu hiyo ya Nokia huku akichaji na ghafla simu hiyo ililipuka na kumsababishia majeraha makubwa ya kifua na mikono yaliyomfanya apoteze fahamu na kukimbizwa hosptial. Hata hivyo baada ya kufikishwa hosptalini hapo baadae msichana huyo alisemekana kupoteza maisha kutokana na majeraha makubwa ya kifua yaliyo sababishwa na mlipuko wa simu hiyo.

Akieleza jinsi ilivyo tokea kaka wa msichana huyo aliye julikana kwa jina moja la Oram alieleza kuwa, dada yake alikuwa akiongea na ndugu na simu iliisha chaji na ndipo dada yake alipoenda kuiweka kwenye chaji huku akiongea na baada ya muda kidogo kulitokea mlipuko mkubwa ambao ulimfanya dada yake kupoteza fahamu na baadae kupoteza maisha akiwa hospitalini.

Advertisement

Kampuni ya HMD Global ambayo ndio wasimamizi na watengenezaji wa simu za Nokia, wamekanusha kwa kusema kuwa, simu hiyo ya haijatengenezwa na kampuni hiyo huku ikidai kuwa simu za Nokia za mwaka huu ni simu zenye ubora na zimetengenezwa kwa ungalifu wa hali ya juu.

Kwa sasa bado polisi nchini humo wanaendelea kufanya uchunguzi, huku mwili wa msichana huyo ukihifadhiwa kwaajili ya kuchunguzwa zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use