in

Haya Ndio Yanayo Tegemewa Kuja kwenye Samsung Galaxy S9

Mambo muhimu yanayo tarajiwa kuja kwenye simu mpya ya Samsung

Haya Ndio Yanayo Tegemewa Kuja kwenye Samsung Galaxy S9

Ni siku kumi tu zimebaki mpaka kutoka kwa simu ya Samsung Galaxy S9 na tayari kwenye mitandao mbalimbali kumefurika tetesi mbalimbali juu ya ujio wa simu hii, lakini je ni vitu gani vinategemewa kuja kwenye simu hii.?

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia baadhi ya vitu ikiwa pamoja na sifa zinazo tegemewa kuja kwenye simu hii mpya ambayo imepanga kuzinduliwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 25 mwezi huu.

  • Kamera

Kwa kuanza tuanze na kamera ambayo ndio sehemu inayotegemewa kuangaliwa sana kwenye toleo hili jipya la Galaxy S9. Simu hii inatarajiwa kuja na kamera mbili za nyuma zikiwa na uwezo wa Megapixel 12 kwa Galaxy S9 Plus na kamera moja kwa Galaxy S9. Sasa tofauti na kamera nyingine kamera hizi zimeboreshwa zaidi na kuongezewa uwezo wa kuchukua picha vizuri hasa wakati wa usiku au kwenye mwanga mdogo.

  • Ulinzi

Mbali na matoleo ya nyumba ya Simu za Galaxy, toleo hili jipya la Galaxy S9 linakuja na ulinzi wa aina mpya ambao unaitwa Intelligent Scan, ulinzi huu ni mchanganyiko wa sehemu muhimu za Facial Recognition pamoja na Iris Scanner zote zikifanya kazi kwa pamoja.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy M51

  • Ujio wa 3D emoji

Sasa hii itakuwa kama ilivyo sehemu ya Animoj kwenye iPhone X na kutumia simu mpya ya Galaxy S9 utaweza kutengeneza Emoji zenye kutembea na kufanya kazi kama ilivyo kwenye simu ya iPhone X.

  • Ujio wa Slow Mo

Hii ni sehemu ambayo itakuwa kwenye kamera na inategemewa kuongeza uwezo wa kamera ya Galaxy S9 kuchukua video za taratibu au Slom Motion.

  • Sifa Nyingine

Sifa zingine ambazo zinategemewa kuja kwenye simu hii mpya ya Samsung Galaxy S9 ni pamoja na kioo cha Inch 5.8 chenye teknolojia ya QHD na Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi), Processor ya Qualcomm Snapdragon 845 (kwa simu za  marekani) na Samsung Exynos 9810 (kwa simu za UK). Pia Samsung Galaxy S9 Plus inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6  na Galaxy S9 itakuwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4.

Na hivyo ndivyo baadhi ya vitu vinavyo tegemewa kuja kwenye kwenye simu mpya ya Galaxy S9 pamoja na S9 Plus. Tutakuwa tukikuletea matangazo ya uzinduzi wa Simu hizo Mubashara kabisa hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.