Programu ya WhatsApp Yafikisha Watumiaji Bilioni 1.5 kwa Mwezi

Kutoka watumiaji Bilioni 1.3 mwaka jana mpaka sasa watumiaji bilioni 1.5
Watumiaji wa WhatsApp Watumiaji wa WhatsApp

Facebook kupitia mkurugenzi wake Mark Zuckerberg, ilitangaza kununua programu ya WhatsApp hapo mwaka 2014 kwa dollar za kimarekani billion $19.

Miaka minne badae thamani ya mtandao huo imepanda na watumiji wake kuongezeka kwa kasi zaidi. Ukilinganisha wakati programu hiyo ina nunualiwa na facebook whatsapp ilikuwa na idadi ya watumiaji zaidi ya milioni 450 lakini hivi leo idadi ya watumiaji wa mtandao huo imeongezeka na kufikia bilioni 1.5

Vile vile mtandao huo wa WhatsApp umeongezeka idadi ya watu wanaotuma meseji hadi kufikia idadi ya meseji zaidi ya bilioni 60 kwa siku moja. Hii ni tofauti kubwa kutoka mwezi wa saba mwaka jana 2017 wakati mtandao huo ulipokuwa na watumiaji bilioni 1.3 kwa mwezi pamoja na watumiaji zaidi ya bilioni 1 kila siku.

Advertisement

Mbali na hayo Mark Zuckerberg, amebainisha kuwa kwa sasa mtandao WhatsApp pamoja na instagram ni mitandao inayo ongoza kwa watumiaji wengi wa sehemu ya Stories ukilinganisha na programu nyingine kama snapchat. WhatsApp na instagram zote zina watumiaji wa stories zaidi ya milioni 300 kila siku kulinganisha na mtandao wa Snapchat ambao unao watumiaji wa Stories milioni 178 kwa siku.

Haya ni mafanikio makubwa sana ya mtandao wa WhatsApp ni wazi kuwa uamuzi wa facebook kununua WhatsApp kwa dollar bilioni $19 ulikuwa ni uamuzi mzuri sana japo kwa kipindi hicho ilikua inaonekana kuwa facebook imelipa pesa nyingi sana. Ni wazi kuwa facebook itanza kurudisha faida yake kwa kutengeneza pesa nyingi zaidi tena ukizangati sasa inayo programu mpya ya WhatsApp ya Biashara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use