Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimae WhatsApp ya Biashara Sasa Yafika Rasmi Tanzania

Sasa unaweza kupakua App ya WhatsApp kwajili ya Biashara kupitia Android
WhatsApp ya Biashara WhatsApp ya Biashara

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu baada ya kuzinduliwa, hatimaye hivi leo WhatsApp ya Biashara imefika rasmi kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Programu hiyo mpya ina husisha urahisi wa mawasiliano baina ya wafanya biashara na watu wa kawaida ambao hutafuta kupata huduma kupitia mitandao ya kijamii. WhatsApp ya Biashara inakuja na vitu mbalimbali ambavyo ni tofauti na programu ya whatsapp ya kawaida kama vile ukurasa maalum wa kibiashara, uwezo wa kujibu meseji haraka au quick replies na mengine mengi.

Advertisement

Lakini kabla hauja amua kutumia WhatsApp ya Biashara ni vyema ujue mambo haya machache muhimu ambayo yataku saidia kupata ufahamu wa programu hiyo.

Ni muhimu kutumia namba ambayo hautumi kwenye WhatsApp ya kawaida kwani utakapo badilisha namba hiyo na kutumia kwenye WhatsApp ya Biashara namba hiyo haito weza kutumika kwenye Whatsapp ya kawaida na hii ni mpaka utakapo anza usajili upya.

Vilevile kama umesajili WhatsApp ya Biashara na imefika wakati wa kuingiza jina la biashara yako ni muhimu sana kuchagua jina halisi la biashara yako kwani jina hilo halitaweza kuja kubadilishwa baadae hii ni mpaka utakapo anza tena hatua za usajili mpya. Na kumbuka kuweka data zako za muhimu kama website picha na vingine vya muhimu ili kuweza kufanya namba yako kuhakikiwa na kuwekewa tiki ya kijani au kuwa Verified

Basi kama umefuata na kusoma yote hayo sasa unaweza kupakua WhatsApp ya Biashara na kujaribu sehemu mpya za programu hiyo kwenye simu yako ya Android. Unaweza kupakua kwa kubofya hapo chini.

WhatsApp Business
Price: Free

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use