Twitter imetangaza kuwa sasa imebadilisha vigezo na mashari ya utumiaji wa mtandao huo, huku ikiwataka watu wenye akaunti zaidi ya moja kuwa makini dhidi ya utumiaji wa mtandao huo.
Katika mabadiliko hayo Twitter imepiga marufuku matumizi ya mitandao mingine kutuma Tweet ya aina moja kwenye akaunti mbalimbali kwa wakati mmoja. Aina hii ya kuposti hufanywa na mitandao mbalimbali (au programu maalum) ambapo humsaidia mtu mwenye akaunti nyingi au akaunti zaidi ya moja kuposti kwenye akaunti zake bila yeye kuingilia au kuposti mwenyewe kwenye mtandao.
Vilevile mabadiliko hayo yamekataza matumizi ya mitandao au programu mbalimbali ambazo zinauwezo wa kulike tweet nyingi kwa wakati mmoja, kufollow akaunti nyingi kwa wakati mmoja, pamoja na kuretweet tweet moja mara nyingi na kwa wakati mmoja.
Twitter imetangaza kuwa vigezo hivyo vipya na masharti vitaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 23 ya mwezi wa tatu mwaka huu 2018, ambapo hadi wakati huo kila mtumiaji anatakiwa awe amesha rekebisha hayo kwenye akaunti zake ndani ya mtandao huo.
Hata hivyo vigezo hivi havita kuwa muhimu kwa wale wanao tumia mitandao au programu mbalimbali kupost tweet moja kwenye akaunti moja. Unaweza kusoma kwa ukamilifu mabadiliko hayo HAPA.