in

LG Yazindua Toleo Jipya la Simu Mpya ya LG V30S ThinQ

Ifahamu hii hapa simu mpya ya LG V30S ThinQ

Simu Mpya ya LG V30S

Mwaka jana kampuni ya LG ilizindua simu yake mpya ya LG V30 ambayo ilikuwa simu bora sana hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kamera. Sasa Kampuni ya LG imerudi tena kupitia mkutano wa MWC 2018 ambapo sasa inakuja na toleo jipya la simu hiyo ya LG V30S.

Simu hii haina tofauti sana na simu ya LG V30, bali simu hii imeongezewa mambo mbalimbali kama vile mfumo wa AI au artificial intelligence ikiwa ni pamoja na muonekano mpya na watofauti kidogo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6 pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835 huku kwa nyuma ikiwa na kamera mbili za nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye uwezo wa kuchukua picha za wide-angle. Kwa mbele LG V30S inakuja na kamera ya Megapixel 5.

Kuna tofauti ndogo sana kwenye simu hii ya LG V30S ThinQ na LG V30 ya mwaka jana na kwa mujibu wa wataalam utofauti ulipo kwenye simu hizi ni sehemu iliyo ongezwa kwenye LG V30S ni sehemu ya AI au Artificial Intelligence ambayo kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.

LG Yazindua Toleo Jipya la Simu Mpya ya LG V30S ThinQ
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.