in

Programu Mpya ya Telegram X ya Android Yaondolewa Play Store

App ya Telegram X kwa mfumo wa iOS bado inapatikana App Store

App Mpya ya Telegram X

Siku za karibuni kampuni ya Telegram kupitia tovuti yake ya Telegram ilitangaza ujio wa App yake nyingine mpya ya Telegram X kwa mifumo ya Android na iOS, lakini baada ya App hiyo kukaa zaidi ya mwezi sasa inaonekana kuwa App hiyo haipo tena kwenye soko la Play Store.

Telegram X
Price: Free

Kwa sasa bado hakuna sababu za kwanini App hiyo imeondolewa kwenye soko hilo lakini inawezekana labda app hiyo imetolewa kwa kukiuka vigezo na mashari ya Google au imeondolewa kwa bahati mbaya au kwa sababu nyingine mbalimbali.

App ya Telegram X kwa upande wa iOS bado inapatikana kwenye soko la App Store na unaweza kuendelea kutumia App hiyo. Kwa mujibu wa tovuti ya Android Police tayari wamesha wasiliana na kampuni ya Telegram kutaka kujua sababu za kuondolewa kwa App hiyo hivyo tutakuleta muendelezo wa makala hii tutakapo pata taarifa zaidi.

Update – App hiyo imerudishwa Play Store, lakini bado hakuna taarifa yoyote kwanini App hiyo iliondolewa kwenye soko hilo. endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.

Kwa sasa kama unataka kuendelea kutumia App hiyo unaweza kupakua App ya Telegram X kupitia tovuti ya APK Mirror.

Hii Hapa App Bora kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.